060-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Kutayammamu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Twahara

 

060-Kutayammamu 

 

Alhidaaya.com

 

 

(Katika mlango huu, nilifaidika sana kutokana na utafiti uliotayarishwa na kaka yangu Twaariq Saalim  (Allaah Amlipe jaza Yake ) kwa ajili ya kujipatia “Master” katika sharia).

 

Kutayammamu Kilugha Na Kisharia [Al-Majmu’u (2/238), Al-Mughniy (1/148) na Al-Mabsuwtw (1/106)]

Kilugha ni kukusudia. Ikisemwa: ،(تيممت فلانا، يممته، تأممته وأممته)inamaanisha: Nimemkusudia fulani.

 

Allaah Mtukufu Anasema:

((ولا تيمموا الخبيث منه تنفقون))

((Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya..)). [Al-Baqarah (2:267)].

 

Ama kisharia, ni kuukusudia mchanga wa juu ya ardhi kwa ajili ya kuhalalika yanayohalalishwa na wudhuu na kuoga.

 

 

Share