Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad: Maana Ya “Kuwa Pamoja Na Wachache Walioongoka Usidanganyike Na Wengi Walioangamia"

 

Maana Ya Kauli:  “Kuwa Pamoja Na Wachache Walioongoka,

Usidanganyike Na Wengi Walioangamia"

 

 Shaykh ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Tunaomba utukirimu kwa kutufafanulia kwa ufupi maana ya maneno ya Fudhwayl bin ´Iyaadhw:  “Fuata Njia ya uongofu na wala haikudhuru wachache wa wenye kuifuata. Tahadhari na njia za upotevu na wala usidanganyike na wingi wa wenye kuifuata.”

 

 

 

JIBU:

 

Ndio. Mtu anatakiwa kukimbilia kufuata Sunnah hata kama watakuwa wachache watu wake. Asidanganyike na njia za batili hata kama watakuwa wengi watu wake. Haki ndio yenye haki kufuatwa hata kama watakuwa wachache watu wake. Batili haijuzu kuingia ndani yake hata kama watakuwa wengi watu wake. Kwa ajili hii imesemekana:

 

“Maajabu sio kwa aliyeangamia ameangamia vipi. Bali maajabu ni kwa aliyeokoka ni vipi ameokoka”

 

Kwa sababu walioangamia ndio wengi na waliookoka ndio wachache. Isistaajabishe wingi wa wenye kuangamia, bali ambalo linatakiwa kustaajabisha ni wingi wa waliookoka. Mtu akimbilie kuwa miongoni mwa wachache waliookoka na atahadhari kuwa miongoni mwa wengi walioangamia.

 

Wachache waliokoka ni wale ambao wanafuata Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa ajili hii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema:

“Hakika yeyote atakayeishi katika nyinyi ataona ikhtilafu nyingi.”

Kana kwamba aliulizwa: “Unatuamrisha nini kuhusu ikhtilaafu hii? Akasema:

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu baada yangu. Shikamaneni nazo bara bara na ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema kutakuwa tofauti nyingi na akaashiria katika kundi moja litakalookoka. Amesema tena:

“Ummah huu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa kundi limoja.” Kukasemwa: “Ni kina nani hao, ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: “Al-Jamaa´ah”.

 

Katika riwaayha nyengine:

 

“... ni wale wataokuwa juu ya yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahabah zangu.”

 

Makundi sabini na mbili yatayokuwa Motoni ni katika Waislamu. Ni wenye kustahiki adhabu. Kundi lililookoka ni lile alilosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

“Ni lile litalokuwa katika yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahabah zangu.”

yaani watakuwa katika njia iliyonyooka na manhaj aliyokuja nayo yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake. Allaah (Ta´aala) Anasema:

 

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

  “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake.    [Al-An’aam: 153]

 

 

Kwa kuwa Njia ya kwenda kwa Allaah (Jalla wa´Alaa) ni moja na ndio ile aliyokuwemo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  na Maswahaba zake. Njia nyinginezo zina upindaji na ni nyingi. Kwa ajili hii ndio maana Allaah Anasema:  

 

  وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ  

Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake.    [Al-An’aam: 153]

 

Kwa kuwa ni nyingi. Upande mwingine haki ni moja tu:

 

 Kauli yake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

“Ummah huu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa kundi limoja.” Kukasemwa: “Ni kina nani hao, ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: “al-Jamaa´ah”.

 

Na pia:

 

“... ni wale wataokuwa juu ya yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahaba zangu.”

 

Na pia:

 

“Hakika yeyote atakayeishi katika nyinyi ataona ikhtilafu nyingi. Hivyo jilazimieni na Sunnah zangu.”

 

Kwa haya yanapata kubainika maneno ya Fudhwayl bin ´Iyaadhw na wengine ambao wamesema pia:

“Fuata njia ya haki hata kama wenye kuifuata watakuwa ni wachache. Tahadhari na kufuata njia ya batili hata kama watakuwa wengi wenye kuifuata.”

 

Baadhi ya Maimaam pia wamesema:

“Kimbilia kuwa miongoni mwa wachache waliookoka na utahadhari kuwa miongoni mwa wengi walioangamia.”

 

Baadhi yao pia wamesema:

 

“Maajabu sio kwa aliyeangamia, ameangamia vipi   Bali maajabu ni kwa aliyeokoka ni vipi ameokoka.”

 

Kwa kuwa waliookoka ni wachache na walioangamia ni wengi.

 

 

[´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad]

 

 

Share