Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad: Hukmu Ya Kuitikia Mwaliko Wa Mzushi

 

Hukmu Ya Kuitikia Mwaliko Wa Mzushi

 

Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Imekuja katika Hadiyth: “Na anayekualikeni muitikieni…” Je, akiwa Mualikaji ni katika Ahlul-Bida’i (Wazushi), je, inapaswa kuitikia (mwaliko huo)?

 

 

JIBU:

 

Hautikwi mwaliko wake ikiwa ni katika Ahlul-Bida’i (Wazushi), au kukiwa katika mwaliko huo kuna bid’ah, au kuna maovu.

Ama ikiwa atakwenda na kuhadharisha bid’ah au kukataza bid’ah, basi hilo ni (jambo) lenye kuruhusiwa.

Ama ikiwa yeye anakwenda (kwenye huo mwaliko) na kula kama kwamba hakuna kilichotokea, basi jambo hilo si sahihi.

 

 

[Sharh Sunan Abiy Daawuwd (580)]

 

 

Share