Shaykh Fawzaan: Kuwaasi Na Kuwalaumu Walii Al-Amr Ni Kuasi Amri Ya Rasuli wa Allaah

 

 

Kuwaasi Na Kuwalaumu Walii Al-Amr Ni Kuasi Amri Ya Rasuli wa Allaah

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mtu anayewaasi Walii Al-Amr (Viongozi wa nchi) na kuwalaumu?

 

JIBU:

 

Yeyote anayekanusha amri ya kiongozi basi hakika amemuamsi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kwani madamu kiongozi hajamuamrisha atende madhambi basi kutokumtii yeye ni kutokmtii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Hali kadhalika kumlaumu kiongozi ni madhehebu ya Khawaarij ambao wanalaumu viongozi na kuwasema vibaya na kuwashawishi watu dhidi yao. 

 

 

Makundi ya vijana wenye hamasa za rabshah walioinuka dhidi ya ‘Uthmaan bin Afaaan hawakufanya hivyo isipokuwa kutokana na chuki iliyovuka mipaka ya ibn Sabaa.  Alianza kukuzugumza katika mikusanyiko ya watu na kuwashawishi watu mpaka mwishowe wajinga kati ya hao watu walianza kughadhibika na wakaishia  kumuua ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) . 

 

Na je mtihani gani Waislamu walitumbika katika kumuua huko?  Jambo hilo llikawafanya nyewele zao kugeua mvi kutokana na kumuua Khalifa na kumpinga na kumpiga vita.”

 

 

[Al-Ijaabaat Al-Muhimmah fiy Mashaakil Il-Mudlahimah]

 

Share