Shaykh Fawzaan: Kutafuta Barakah Katika Nyumba Mpya Kwa Kuchinja

 

Kutafuta Barakah Katika Nyumba Mpya Kwa Kuchinja

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Shaykh mheshimiwa, baadhi ya watu huchinja mlangoni wanapojenga nyumba mpya wakikusudia kutafuta baraka na kujikinga na jicho baya. Na mtu huyo hajui kuwa kuchinja huko kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki. Je, mtu huyo atakuwa amekufuru?

 

 

JIBU:

 

Mtu huyo aamrishwe kutubia na aambiwe kuwa hiyo ni shirki, kwa hiyo lazima arudi kutubia kwa Allaah! Kwa sababu anayetenda shirki kama hiyo ni mshirikina.

 

[Shaykh Fawzaan, Silsilatush-Sharh Rasaail (Uk. 120)]

 

 

Share