Du'aa: Kuna Du'aa Sahihi Wakati Wa Kufuturu?

Je, Kuna Du’aa Sahihi Wakati Wa Kufuturu:

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni ipi hukmu ya Hadiyth hii:

ذَهَـبَ الظَّمَـأُ، وَابْتَلَّـتِ العُـروق، وَثَبَـتَ الأجْـرُ إِنْ شـاءَ اللهُ

“Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na yamethibiti malipo Allaah Akipenda”

 

Je, kuna du’aa yoyote iliyothibiti ya kwa ajili ya kufungulia swawm?

 

 

JIBU:

 

Hiyo Hadiyth si sahihi.

 

Mwenye kufunga du’aa yake inaitikiwa, ikiwa ataomba wakati wa kufuturu au kabla ya kufuturu.

 

Allaah Anasema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾

60. Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike. [Ghaafir: 60]

 

Kadiri mja anavyohitaji msaada na kujikurubisha karibu na Allaah ndivyo du’aa yake inavyopokelewa.

 

Hadiyth uliyoitaja ni dhaifu kwa sababu (katika wapokezi kuna) Marwaan bin Saalim Al-Muqfayaa hajulikani.

 

Na Allaah Ni Mjuzi Zaidi.

 

 

Share