Skip to main content

Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kuwafananisha Watoto Na Malaika

Kuwafananisha Watoto Na Malaika Haijuzu

Al-Lajnah Ad-Daaimah

Alhidaaya.com

SWALI:

”Ni nini hukumu ya kuwafananisha watoto na Malaika, kwa sababu katika lugha yetu tunasema kuwa watoto ni Malaika?”

JIBU:

Haifai. Hili ni kosa kubwa ambalo watu wengi wanaangukia na hakuna hoja wala mazingatio ya kudai kwao kwamba wanakusudia kuwa watoto hawana dhambi kama vile Malaika.

Wa bi-LLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa: Fatwa (16)]