Al-Lajnah Ad-Daaimah: Maulidi: Kula Nyama Inayochinjwa Kwa Ajili Ya Maulidi Na Vinginevyo

 

Kula Nyama Inayochinjwa Kwa Ajili Ya Maulidi Nabiy Na Vinginevyo Vya Maulidi

 

Al-Lajnah Ad-Daa'imah

www.alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Je, inajuzu kula nyama inayochinjwa kwa ajili ya Mawlid Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vinginevyo vya Mawlid?

 

 

JIBU:

 

Kinachochinjwa kwa ajili ya Mawlid Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au waliyy (mtu mwema kaburini), kwa ajili ya kumuadhimisha basi hayo ni katika yanayochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah na hivyo ni shirki; hivyo haijuzu kabisa kuila.

Na imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

لعن الله من ذبح لغير الله

“Allaah Amemlaani anayechinja kwa asiyekuwa Allaah.”

 

Wa biLLaahit-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam

 

[Fatwa (217) – Al-Lajnah Ad-Daaimah]

 

 

Share