Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Wali Wa Zaafaraan Na Kuku Wa Kupaka

 

 

Vipimo

Wali:

Mchele - 3 Vikombe

Kitunguu kiichokatwa - 1

Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande -  1       

Mafuta -  ¼ Kikombe

Zaafarani  - 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka

Chumvi  - 1 kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
 2. Tia pili pili boga.
 3. Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
 4. Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
 5. Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.

Kuku

Kuku Mzima  -1

Mayai  ya kuchemsha  -  6

 

Namna Ya  Kupika Kuku

 1. Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
 2. Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
 3. Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando

Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi

Kitunguu - 1

Nyanya iliyokatwa vipande  -   1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu

Garam Masala - ½ kijiko cha supu

Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Pilipili masala ya unga  -  ½ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo  -  1 kijiko cha supu

Nazi ya unga - 1 kikombe

Maji ya ukwaju - ¼ kikombe cha chai                                                                                                                                

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
 2. Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
 3. Tia thomu na tangawizi.
 4. Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
 5. Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
 6. Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
 7. Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
 8. Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
 9. Mtie kwenye oveni kidogo.

Kupakuwa katika Sinia

 1. Pakuwa wali kwanza katika sinia
 2. Muweke kuku juu ya wali.
 3. Pambia mayai 

 

 

 

 

Share