Makaroni Ya Kuku Na Bashamel (Sosi Nyeupe)

Makaroni Ya Kuku Na Bashamel (Sosi Nyeupe)

Vipimo   

Makaroni (aina yoyote) - 500 gms

Kuku:

Nyama ya kuku bila mafupa

iliyokatwa ndogo ndogo -1LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga  ya unga - 1 kijiko cha chai

chumvi - kiasi

Vipimo vya Sosi

Mafuta ya kupikia - 1/4 kikombe

Nyanya – kata ndogo ndogo - 4

Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu

Kechapu ya nyanya (tomato ketchup) - 5 vijiko vya supu

 

Supu ya kuku ya vidonge:

Mraba ya supu ya kuku au nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

 

Viungo vya Kiitali ukipenda

 

(Italian spices; Oregano, mint, thyme) - 1 kijiko cha supu

 

Namna ya kutayarisha

 1. Mtie kuku chumvi, pilipili manga, thomu, mpike awive. (Unaweza kutumia kidari au sehemu yoyote ya kuku, ukishaipika utoe mafupa na uchambue nyama ndogo ndogo)
 2. Epua weka kando.
 3. Tia mafuta katika sufuria, kaanga nyanya, tia nyanya kopo, kechapu, viungo vya kiitali, pilipilimanga , chumvi na kidonge cha supu (Maggi cube).
 4. Pika hadi sosi iwe tayari isiwe nzito sana, ongeza maji 1/2 kikombe.

*Vipimo vya Bashamel 

 

Unga mweupe - 1/2 kikombe

Siagi (butter) - 3 vijiko vya supu

Maziwa - 2 vikombe vikubwa (mugs)

Kidonge cha supu (Maggi cube) - 1

 

Namna ya kutayarisha

 1. Tia unga katika sufuria.
 2. Tia siagi kaanga kidogo ubadilike rangi unga uwe rangi ya hudhurungi hafifu. (light brown)
 3. Tia maziwa koroga kwa mwiko wa kupigia mayai au tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage ili uondoshe madonge.
 4. Tia kidonge cha supu (Maggi cube) kisha rudisha katika moto kidogo uipike sosi. Isiwe nzito sana iwe kama kastadi na kama nzito sana ongeza maziwa. 
 5. * Iwe kazi ya mwisho kutayarisha sosi, umwagie katika makoroni ukiwa tayari umeshapanga kila kitu.

Vya kumwagia ndani na juu ya makaroni

 

Jibini zote ziwe zimekunwa (grated)

Jibini ya cheddar (cheddar cheese) - 200 – 250 gm

Jibini ya mazorella (mozorella cheese) - 200 –250 gm

 

Utakuwa umetayarisha vitu hivi viwe tayari

 

Kuku aliyepikwa na kuchambuliwa

Sosi ya nyanya

Makaroni yaliyochemshwa yakaiva

Sosi ya Bashamel

Jibini iliyokunwa (shredded cheese)

Kumalizia kupika makaroni

 1. Panga nusu makaroni katika bakuli au trea ya kupikia katika oveni.
 2. Tia nusu ya sosi ya nyanya
 3. Tia nusu ya kuku aliyechambuliwa
 4. Tia nusu ya jibini iliyokunwa
 5. Rudia kupanga tena kwa mpangilio huo huo.
 6. Malizia kwa kumwagia sosi ya bashamel hakikisha inaingia pande zote na ndani ya makaroni.
 7. Pambia kwa viungo vya kiitali au naanaa (mint) iliyokatwa ndogo ndogo.
 8. Pika katika oveni moto wa 350-400º kwa muda wa dakika 15-20 hadi jibini sosi ya bashamel iwive.
 9. Epua ikiwa tayari kuliwa.

 

 

Share