Pai Ya Viazi Na Nyama Ya Kusaga

Pai Ya Viazi Na Nyama Ya Kusaga

Vipimo

Nyama ya kusaga - 1½ lb (ratili)

Kitunguu - 1 Kikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 Kijiko cha supu

Mboga upendayo

(karoti, mahindi, na kadhalika) - 1- 2 Kikombe

Viazi - 1½ - 2 lb (ratili)

Siagi - ½ Kikombe

Kidonge cha supu kilichoyeyushwa - ½ Kikombe maji

Worcestershire sauce au yoyote nyingine - 1 Kijiko

Chumvi - kiasi

Mchanganyiko wa bizari - 1 Kijiko cha supu

Jibini (cheese) ya iliyochunwa (grated) - 1 gilasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Menya maganda ya viazi na katakata, kisha chemsha katika maji yenye chumvi hadi viwive.
  2. Wakati viazi vinaiiva, yeyusha nusu ya ile kipimo cha siagi katika sufuria kisha kaanga kitunguu hadi ilainike.
  3. Kisha tia thomu na tangawizi.
  4. Halafu tia nyama ya kusaga na ukaange hadi isiwe nyekundu tena.
  5. Weka mboga, chumvi na bizari zilizobakia na iachie moto mdogo kwa muda iive vizuri.
  6. Ponda viazi pamoja na ile siagi iliyobakia, kisha ongeza chumvi na pilipili manga ikiwa haijakolea.
  7. Tandaza kwanza viazi kisha mchanganyiko wa nyama katika treya ya oveni kisha tandaza tena viazi vilivyopondwa kwa kutumia uma ili iwe na dizaini upendayo.
  8. Mwagia jibini (cheese) juu yake.
  9. Pika katika oveni yenye moto wa 400° kwa muda wa dakika 30 hivi na ubadilisha moto wa juu katika dakika 5 za mwisho ili igeuke rangi ya kupendeza juu.
  10. Epua na tayari kuliwa.
Share