Makaroni Ya Nyama Ya Kusaga Kwa Jibini Na Sosi Ya Bashamel

Makaroni Ya Nyama Ya Kusaga Kwa Jibini Na Sosi Ya Bashamel

 

 

Vipimo

 

Makaroni (aina yoyote) - 1 Pakti (950) gms

Vipimo Vya Sosi

Nyama ya kusaga - 1 Kilo

kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya chai

Pilipili manga  ya unga - 1 kijiko cha chai

Vitumguu maji - 2

chumvi - kiasi

Mafuta ya kupikia - 1/4 kikombe

Sosi ya macaroni - 1 kopo (680) gm

Mraba ya supu ya nyama - kidonge 1 (au supu yenyewe kiasi kidogo tu cha kutia ladha lakini hakikisha supu isizidishe kipimo).

Garam masala - 1 Kijiko cha chai

Dania ya unga - 1 Kijiko cha chai

Kotmiri - 2 Vijiko vya Supu

Pilipili ya unga - 1 Kijiko cha chai

Ndimu - 2 Vijiko vya supu                                                    

Ikibidi: unaweza kutumia nyanya ya kopo badala ya sosi ya makaroni

 

Namna Yakutayarisha

 1. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitungu, tia thomu na tangawizi kisha tia nyama ya kusaga vilevile mbichi wacha ikaangike kisha tia bizari zote isipokuwa sosi ya makaroni.
 2. Halafu tia sosi ya makaroni wacha ichemke mpaka sosi iwe mzito.

Vipimo Vya Bashamel

 

Unga mweupe - 4 Vijiko vya supu

Siagi (butter) - 3 vijiko vya supu

Maziwa - 1 lita

Pilipili manga - ½ kijiko cha chai

Mayonezi - 2 Vijiko vya supu

Jibini iliyokunwa(Grated Cheese) - 2 Vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha

 1. Tia unga katika sufuria siagi na mafuta kaanga kidogo .
 2. Tia maziwa koroga kwa mwiko  na usage ili uondoshe madonge mpaka uwe mzito kama uji.
 3. Kisha tia mayonezi , pilipili manga na jibini ilikwanguliwa.
 4. * Iwe kazi ya mwisho kutayarisha sosi, umwagie katika makoroni ukiwa tayari umeshapanga kila kitu.

Vya Kumwagia Ndani Na Juu Ya Makaroni

 

Jibini zote ziwe zimekunwa (grated)

Jibini ya cheddar (cheddar cheese) - 200 – 250 gm

Jibini ya mazorella (mozorella cheese) - 200 –250 gm

 

Utakuwa Umetayarisha Vitu Hivi Viwe Tayari

 1. Sosi ya nyama ya kusaga
 2. Makaroni yaliyochemshwa yakaiva
 3. Sosi ya Bashamel
 4. Jibini iliyokunwa (shredded cheese)
 5. Mapilipili mboga ya rangi tofauti.

Kumalizia Kupika Makaroni

 1. Panga nusu makaroni katika bakuli au trea ya kupikia katika oveni.
 2. Tia nusu ya sosi ya nyama
 3. Tia nusu ya jibini iliyokunwa
 4. Tia tena makaroni yaliyobaki
 5. Malizia kwa kumwagia sosi ya bashamel hakikisha inaingia pande zote na ndani ya makaroni.
 6. Pambia kwa Mapilipili mboga yaliyokatwakatwa.
 7. Malizia juu yake jibini iliyobaki
 8. Tia kwenye oven kwa moto wa 350 ˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 20 mpaka jibini iyayuke
 9. Epua ikiwa tayari kuliwa.

 

Kidokezo:

 

Unaweza kutumia sosi ya pasta ya tayari ila uongeze nyama ya kusaga uliyoikausha kwa viungo. 

 

 

Share