Makaroni Ya Nyama Ya Kusaga, Brokoli, Karoti Na Pilipili Boga

Makaroni Ya Nyama Ya Kusaga, Brokoli, Karoti  Na Pilipili Boga

Vipimo

Makaroni - 500 gm

Nyama ya Kusaga - 1 ratili

Vitunguu - 2

Nyanya - 3

Nyanya kopo (tomato paste) - 3 vijiko vya supu

Brokoli - 1 msongo (bunch)

Kitunguu Saumu(thomu/garlic) kilosagwa - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Bizari ya oregano [Italian spice] - 1 kijiko cha chai

Parsely  (aina ya kotmiri) - 2 misongo (bunches)

Sosi ya soya - 2 vijiko cha supu

Mafuta - ¼ kikombe cha chai

Karoti - 2

Pilipili mboga - 1

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha Makaroni kama inavyoeleza katika paketi, chuja maji weka kando.
  2. Katakata vitunguu, nyanya vipande vidogo vidogo weka kando
  3. Chambua brokoli weka kando.
  4. Katakata parsley ndogo ndogo (Chopped) weka kando.
  5. Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kidogo tu.
  6. Tia nyama, kitunguu thomu, bizari zote endelea kukaanga hadi nyama iwive.
  7. Tia nyanya pamoja na nyanya kopo, tia  brokoli, parsely, sosi ya soya  endela kukaanga kidogo tu.
  8. Tia makoroni changanya vizuri.
  9. Pakuwa katika bakuli, mwagia karoti na pilipili mboga zilokatwa katwa ikiwa tayari.

 

 

                                                                  

 

 

 

 

Share