Kachumbari Ya Asili

Kachumbari Ya Asili

 

 

Vipimo:

               

Vitunguu –  kiasi 4

Nyanya -  kiasi 3

Pilipili mbichi – kiasi 2

Chumvi -kiasi

Ndimu – 2 kamua

 

Namna Ya Kutayarisha:

 

  1. Menya vitunguu ukate slesi nyembamba.
  2. Tia chumvi kwa wingi kiasi uoshe na uchuje vitunguu.
  3. Mimina katika bakuli, kisha katiakatia nyanya na pilipili mbichi.
  4. Koleza chumvi na tia ndimu ikiwa tayari kuliwa khasa kwa pilau.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share