Saladi ya Croutons

Saladi ya Croutons

Vipimo

Saladi ya Kijani (Green Lettuce) - 1/4  msongo (bunch)

Saladi Nyekundu (Red lettuce) - 1/4     msongo

Tango - 1

Figili ya kiazi (radish) - 7

Pilipili Boga - 1

Vitunguu maji vyeupe vya saladi - 1 kikubwa

Zaituni za kijani -  1/4   kikombe cha chai

Zaituni nyeusi - 1/4  kikombe cha chai

*Croutons - 2 vikombe vya chai

(Mikate Ya Ki Italy iliyokatwa vipande vidogo vidogo vya mraba)

* Dressing Ya Ki Italy -  1/2 kikombe

* Unaweza kutumia za tayari au tengeneza mwenyewe kwa kufanya ifautavyo:

Croutons:

Vipimo:

Slaisi za mkate - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1

Mafuta - Ya kukaangaia

Namna ya Kutayarisha:

 1. Nyambua mikate pembeni uweke kando (Tumia katika upishi wa katlesi kama bread-crumbs)
 2. Katakata mikate vipande vidogo vidogo vya mraba saizi ya sentimeta  moja (1 cm cube)
 3. Tia mafuta katika karai ndogo
 4. Tia thomu kaanga kidogo kisha tia vipande vya mikate ulivyovikata ukaange hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) isiyokoza.
 5. Toa weka kando kwa ajili ya kuchanganya na saladi.
 6. Dressing ya Kiitali

Vipimo:

Mafuta ya Zaytuni - 1/4 kikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 3 chembe

Pilipili nyekundu ya unga - 1/4 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Haradali ya powder au iliyo tayari

(Mustard powder au sosi ya mustard) - 1 kijiko cha chai

Herbs za Kiitali (kama Nanaa kavu) - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 2 Vijiko vya supu

Changanya vitu vyote pamoja ikiwa tayari.

Namna ya Kutayarisha Saladi

 1. Katika bakuli kubwa au sahani ya saladi, katakata majani ya saladi zote za aina mbili.
 2. Katakata tango, pilipili boga figili kiazi, kitunguu.
 3. Changanya na zaituni zote.
 4. Changanya na Croutons.
 5. Karibu na kula mwagia dressing ya Ki Italy uchanganye vizuri.

 

 

 

 

Share