Bilingani Kwa Sosi Ya Nyanya Na Ukwaju

Biringani Kwa Sosi Ya Nyanya Na Ukwaju 

 

Vipimo

              

Bilingani - 2 Makubwa

Vitunguu maji - 2 vya kiasi

Nyanya -  2 za kiasi

Kitunguu saumu (thomu/saumu) uliyosagwa - 1 ½  Kijiko cha chai

Pilipili mbichi iliyosagwa (au kukatwa ndogondogo) - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Ukwaju - 1 Kikombe cha chai

Vitunguu vya kijani (spring onions) -  mche mmoja

Mafuta ya kukaangia mabilingani               

 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
 
1.   Kata mabilingani nusu kwanza, kisha kata vipande kwa urefu vya kiasi 1.5 cm
2.  Kaanga mabilingani katika mafuta ya moto kabisa, mpaka yageuke rangi.  Epua na yaweke katika chujio yachuje mafuta.
3.  Kataka vitunguu vidogo vidogo (chopped), kaanga mpaka viwe vyekundu kidogo.
4.  Tia Thomu kaanga kidogo tu.
5.  Tia nyanya zilizokatwa ndogo ndogo (chopped) endelea kukaanga mpaka ziwe laini, ukiongeza pilipili mbichi iliyosagwa na chumvi.
6.  Yapange mabilingani katika sahani au bakuli la kupakulia na mwaga rojo ulilokaanga juu yake.
7. Mwagia ukwaju na changanya vizuri kwa pole pole yasivurugike mabilingani.
8.  Pambia kwa vitunguu vya kijani (spring onions) viliyokatwa vidogo vidogo (chopped) – Tayari kuliwa.
 
 
Kidokezo:  
 
Ni nzuri sana kuliwa na mikate mikavu kama   mkate wa ufuta  au  Naan  au mkate wa Ki-Lebanon (Pita Pain)
 
 

 

 

 

 

Share