Buns Za Sukari

Buns Za Sukari

  

Vipimo 

Unga - 3 Vikombe vya chai

Maziwa - 1 Kikombe cha chai

Sukari - ¼ Kikombe cha chai 

Siagi -  ¼ Kikombe cha chai

Chumvi -  ½ Kijiko cha supu

Yai - 1

Hamira -  2 ¼ Vijiko vya chai (pakiti 1)

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika kibakuli changanya sukari na ½ kikombe ya maziwa yaliyo vuguvugu, kisha tia hamira, koroga na iwache dakika 5 hivi.
  2. Halafu tia yai na yale maziwa ½ kikombe yaliyobakia na siagi iliyoyeyushwa.
  3. Katika bakuli jengine, changanya unga na chumvi kisha ongezea ule mchanganyiko wa hamira.
  4. Kisha ukande unga baada ya kuinyunyizia unga ili usishike.
  5. Ukipenda unaulaza unga firijini kuongeza ladha au unafanya viduara kama 16 na kuziweka kwenye trei ya kuchomea iliyopakwa siagi.
  6. Ziache pahali penye joto hadi ziemuuke.
  7. Washa  oveni moto wa 350º.
  8. Piga yai na kijiko kimoja cha maziwa, kisha pakiza juu kabla hujachoma.
  9. Vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 au mpaka zibadilike rangi na kuwa tayari.

 

 

Share