025-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Furqaan Aayah 70: إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

025-Asbaab Nuzuwl Al-Furqaan Aayah 70

 

 

 

Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.  [Al-Furqaan (25:70)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنِي سَعِيدُ بْنُ جُبَيْرٍ، أَوْ قَالَ حَدَّثَنِي الْحَكَمُ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ أَمَرَنِي عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبْزَى قَالَ سَلِ ابْنَ عَبَّاسٍ عَنْ هَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ، مَا أَمْرُهُمَا: ((‏وَلاَ تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ)) ((‏وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا‏))‏ فَسَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ فَقَالَ لَمَّا أُنْزِلَتِ الَّتِي فِي الْفُرْقَانِ قَالَ مُشْرِكُو أَهْلِ مَكَّةَ فَقَدْ قَتَلْنَا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ، وَدَعَوْنَا مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ، وَقَدْ أَتَيْنَا الْفَوَاحِشَ‏.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ ‏((‏إِلاَّ مَنْ تَابَ وَآمَنَ‏))‏ الآيَةَ فَهَذِهِ لأُولَئِكَ وَأَمَّا الَّتِي فِي النِّسَاءِ الرَّجُلُ إِذَا عَرَفَ الإِسْلاَمَ وَشَرَائِعَهُ، ثُمَّ قَتَلَ فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ‏.‏ فَذَكَرْتُهُ لِمُجَاهِدٍ فَقَالَ إِلاَّ مَنْ نَدِمَ‏.‏

Ametuhadithia ‘Uthmaan bin Abiy Shaybah, ametuhadithia Jariyr toka kwa Mansuwr, amenihadithia Sa’iyd bin Jubayr na amesema, amenihadithia Al-Hakam toka kwa Sa’iyd bin Jubayr, amesema: ‘Abdur-Rahmaan bin Abzaa aliniamuru akaniambia: Muulize Ibn ‘Abbaas kuhusu Aayah hizi mbili (zifuatazo) Zimekaaje hizi?

 

وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِف فِّي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنصُورًا ﴿٣٣﴾

Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki. Na atakayeuliwa kwa kudhulumiwa, basi Tumemfanya mrithi wake awe na mamlaka.  Lakini asipindukie mipaka katika kuua. Hakika yeye atasaidiwa (kwa shariy’ah).   [Al-Israa (17: 33)]

 

Na,

 

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾

Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, ni mwenye kudumu humo na Allaah Atamghadhibikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu. [An-Nisaa (4:93)]

 

 

Nikamuuliza Ibn ‘Abbaas akasema: Ilipoteremshwa ile ambayo iko kwenye Al-Furqaan [Aayah ya 70], washirikina wa Makkah walisema: Hakika sisi tumeua nafsi ambayo Allaah Ameharamisha (kuiua), tumeomba mwabudiwa mwingine pamoja na Allaah, na pia tumefanya machafu. Hapo Allaah Akateremsha:

 

إِلَّا مَنْ تَابَ إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.  [Al-Furqaan (25:70)]

 

Ama Aayah iliyoko kwenye [Suwrat] An-Nisaa, ni kwamba mtu akiujua vyema Uislamu na Shariy’ah zake, kisha akaua (kwa kusudi), basi malipo yake ni Jahannam adumu humo milele. Nikamweleza hilo Mujaahid naye akasema: Ila kwa aliyejuta.  [Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Nane ukurasa wa 167]

 

[Hadiyth ameirejesha katika Tafsiyr Al-Furqaan Mujallad wa Kumi ukurasa wa 12, na imekusanywa na Muslim katika Mujallad wa Kumi na Nane ukurasa wa 159, Abu Daawuwd katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 168, na Ibn Jariyj katika Mujallad wa Kumi na Tisa ukurasa wa 42]
 

 

Share