Imaam Ibn Baaz: Inafaa Kutumia Simu Katika Swillat Rahm (Kuunganisha Undugu)?

Inafaa Kutumia Simu Katika Swillat Rahm (Kuunganisha Undugu)?

 

   Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

 

Je inafaa Swillat Rahm (kuunga undugu) kupitia simu?

 

 

JIBU:

 

Naam, hii ni katika Swillat Rahm (kuunganisha undugu), mazungumzo ya simu na maandishi -SMS- hivi vyote ni katika Swillat Rahm, kuwa mtu anaandika kumuandikia ndugu yake ama baba yake mdogo au jamaa yake yoyote yule, akiwa anamuulizia kuhusu afya yake ama hali yake kwa ujumla, ama akampigia simu na kuongea nae, hayo yote ni mambo mazuri na yote ni katika Swillat Rahm (kuunganisha undugu).

 

[Fataawaa Imaam Ibn Baaz:  Nuwr ‘Ala Ad-Darb]

 

Share