Imaam Ibn Baaz: Kuweka Qur-aan Chini Ya Mto Kwa Ajili Ya Kinga, Kuvaa Hirizi Shingoni

 

 Hukmu Ya Kuweka Qur-aan Chini Ya Mto Wa Mtoto

Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuvaa Hirizi Shingoni

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, inajuzu kuweka Qur-aan chini ya mto wa mtoto na kuwavalisha hirizi kwenye shingo zao?

 

 

 

JIBU:

 

 

Haijuzu kuweka Qur-aan chini ya mto iwe kwa mtoto au kwa mwengine yeyote.

Kwa sababu kufanya hivyo ni kuishushia hadhi Qur-aan na pia ni itikadi ambayo mtu anaitakidi kua kufanya hivyo kunamkinga na balaa mtoto au hao wengine; na hili ni kosa, halina asili.

Hakika linalozuia (linalokinga) kwa idhni ya Allaah, ni zile kinga za kishariy’ah. Ni kuwa (kinachotakiwa) mama yake au baba yake kumuombea kinga (ya du’aa) kwa kusema:

 

أعيذك بكلمات الله التامة من كل شيطان وهامة ومن كل عين لامة

“Nakuombea kinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia, kutokana na kila Shaytwaan na vitimbi vyake, na kutokana na kila jicho lenye kudhuru.”

 

Kama alivyokuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwaombea kinga Al-Hasan na Al-Husayn kwa kinga hii akisema:

 

“Nawaombea kinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia, kutokana na kila Shaytwaan na vitimbi vyake, na kutokana na kila jicho lenye kudhuru.”

 

Ama kuweka Msahafu chini ya mto wa mtoto au mtu mzima, hii haijuzu kwa sababu ni kukidhalilisha Kitabu cha Allaah, na ni itikadi potofu isiyo na asili.

 

Na kadhaalika, kutundika chochote kile, au kutundika Aaayah za Qur-aan, au hirizi katika shingo la mtoto au mtu mzima au mgonjwa; haya yote hayajuzu vilevile, kwa sababu ni katika mlango wa kutundika hirizi ambao umekatazwa.

Amesema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

“Atakayetundika hirizi, basi Allaah Hatomtimizia.”

 

Na amesema:

 

“Atakayetundika hirizi, basi atakuwa amefanya shirki.”

 

Kwa hivyo, haijuzu kutundika hirizi ambayo zinatengenezwa kwa kutumia Aayah za Qur-aan zenye kuandikwa, au kwa kutumia susu (ganda za konokono) au mifupa, au kutumia vingine visivyo hivyo kwa yale wanayofanya baadhi ya watu.

 

Hata ikiwa itatumiwa Aayah za Qur-aan kwa usahihi, haijuzu kuzitundika, bali Qur-aan inatakiwa isomwe kwa ajili ya ponyo. Anasomewa mgonjwa kwa kuombewa kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) apate afya.

 

Ama kufanywa ni kitu cha kutundikwa kwenye shingo au kufungwa juu ya mkono karibu na bega iwe kwa mtu mzima au kwa mtoto, haijuzu. Na haya ni katika mambo ya hirizi yaliyoharamishwa na Allaah (Jalla wa ‘Alaa) kuyafanya.

 

[Mawqi’ Imaam Ibn Baaz ]

 

 

Share