Imaam Ibn Baaz: Kupiga Picha Na Kuweka Kwa Ajili Ya Kumbukumbu

Kupiga Picha Na Kuweka Kwa Ajili Ya Kumbukumbu

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nnapokwenda kutembea sehemu kadhaa pamoja na kundi la marafiki huwa napiga picha kuziweka kama kumbukumbu. Nini hukmu ya kupiga picha kwa ajili hii?

 

 

JIBU:

 

Hukmu ya kupiga picha kwa ajili hii ni haramu yaani ikiwa picha ni yenye roho (bin Aadam au mnyama).

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watu watakaoadhibiwa vikali Siku ya Qiyaamah ni wenye kuchora picha.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Pia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelaani wachoraji picha.

 

Ama kupiga picha vitu ambavo havina roho kama gari, ndege, miti n.k., hivi hakuna ubaya.  Wa biLLaahi At-Tawfiyq.

 

 

[Fataawa Islaamiyyah (8/125)]

 

 

Share