Ijue Itikadi Ya Shia Ithnaa-'Ashariyah (Ithnasheri)
Ijue Itikadi Ya Shia Ithnaa –‘Ashariyah (Ithnasheri)
Imefasiriwa Na Muhammad Faraj (Rahimahu Allaah)
Hakika shukrani zote ni zake Allaah. Tunaomba maghfira kutoka kwake, tunamtegemea Yeye peke yake, na tunajikinga kwake kutokana na shari za nafsi zetu na amali zetu zilizo ovu. Yule ambaye Allaah atamuongoza, basi hapana anayeweza kumpoteza, na yule aliyepotoka asitake kufuata uongofu wa Allaah, basi hatopata mwengine wa kumuongoza.
Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah Peke yake asiye na mshirika, na nashuhudia kuwa Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni Nabiy wake na Rasuli wake.
Hakika ya maneno bora ni yale ya Allaah, na hakika ya uongofu bora ni wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na shari ya mambo ni uzushi, na kila uzushi ni Bida-a, na kila Bida-a ni upotofu (upotevu), na kila upotofu mahali pake ni Motoni.
Ndugu yangu msomaji wa maudhui haya, ujuwe ya kuwa mazungumzo haya si juu ya Mashia, bali ni juu ya Mfundisho ya madhehebu yao, pamoja na Itikadi iliyomo ndani ya vitabu vyao. Tunakuomba uyasome pamoja nasi kwa roho iliyotakasika na kwa insafu.
Tuingie moja kwa moja katika maudhui yetu:
Mashia, wamo miongoni mwao wasiojuwa chochote, na wamo wanavyuoni pia. Lakini maudhui yetu ni makubwa sana kupita hivi, kwani sisi tunataka kuzungumza juu ya Ushia kama madhehebu na hatutaki kuzungumza juu ya Mashia kama watu wa kawaida ambao haya ni madhehebu yao, bali sisi leo tunataka kuzungumza juu ya mafundisho ya madhehebu haya ya Kishia.
Shia Al-Imaamiyah (Ithnaa-’Ashariyah):
Hawa ni wale wanaosema kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ni Imam wa mwanzo baada Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufariki dunia, na kwamba Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alimnyang’anya na kumdhulumu Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ukhalifa wake, na akafanya hivyo hivyo ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu), na akafanya hivyo tena ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu).
Mashia Wanawagawa Swahaba Sehemu Mbili:
Sehemu ya kwanza: Waliowaunga mkono Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa), na hawa ndio Swahaba wengi sana.
Sehemu ya pili: Wale ambao hawakuridhika nao, wakakataa kufuata na wakaona kuwa Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wamemnyang’anya Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ukhalifa wake na idadi yao ni Swahaba watatu (Radhwiya Allaahu ‘anhum).
Mashia wamekhitalifiana juu ya idadi ya Swahaba hawa, na juu ya majina yao, lakini wengi wao wanasema kuwa walikuwa watatu tu, nao ni Salman Al Farsiy na Al Miqdaad bin Al Aswad na Abu Dhar Al Ghafariy (Radhwiya llahu anhum).
Kwa ajili hiyo zimepokewa riwaya nyingi za Kishia kuwa Swahaba wote walirtaddi (walitoka katika dini baada ya kufa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa Salman na Al Miqdaad na Abu Dhar (Radhwiya Allaahu ‘anhu), na zimepokelewa baadhi ya riwaya za Kishia kuwa Swahaba wote wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walirtaddi isipokuwa watatu tu, na wakatajwa watatu hao kisha wakaongezwa juu yao Ammar bin Yaasir na baadhi chache ya Swahaba wengine (Radhwiya Allaahu ‘anhu).
Kwa hivyo Mashia wanasema kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ndiye aliyestahiki kuwa khalifa baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini wakakhitalifiana baada ya hapo juu ya nani awe Imamu baada ya Aliy na baada ya Al-Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na wakakhitalifiana khitilafu kubwa sana nani awe Imamu baada ya Ja’afar Al Sadq na pia baada ya Al-Hasan Al Askari.
Inajulikana kuwa Mashia walikuwa wakikhitalifiana kila Imamu wao anapokufa, lakini khitiliafu kubwa ilikuwa baada ya Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa sababu baadhi ya Mashia walikuwa wakiitakidi kuwa Ali (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hawezi kufa na kwamba angali hai, na kwa ajili hiyo wakaukataa umimu wa Al-Hasan bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu), lakini wengi wao waliukubali uimamu wake.
Khitilafu hizo ziliendelea mpaka ulipofika wakati wa uimamu wa Al-Hasan al Askari (huyu ni Imamu wao wa kumi na moja), hapo wakakhitalifiana juu ya nani awe imamu baada yake. Wengine wakasema kuwa yeye ndiye Imam wa mwisho, na wengine wakasema Imamu wa kumi na mbili ni mwanawe (wakatunga hadiyth kuwa alikuwa na mwana juu ya kuwa Al Askari huyu hakuwa na mwana).
Na mwana huyo waliyemtungia hadiyth kuwa alizaliwa, wakati dalili zote zinasema kuwa hajapata kuzaliwa, ndiye Imamu anayesubiriwa ‘Al Muntadhar’, wanayesema kuwa ni mtoto wa Al-Hasan Al Askari (Imamu wa kumi na moja wanaosema kuwa wanamsubiri atokea pangoni. Maana wanaitakidi kuwa mtoto wa huyo wa Al Askari mara baada ya kuzaliwa kwake aliingia pangoni mahali panapoitwa Samurra, na hajatoka mpaka leo, na wao wanamsubiri mpaka hiyo siku atakayotoka.
(Mashia wanakwenda huko kwa wingi kufanya ziara na wanapofika hapo hupiga kelele huku wakiita: ‘(Ajjil ajjil - Fanya haraka utokeee, kwani dunia imejaa dhulma.’) Wengine wakasema kuwa uimamu ulikuwa wa Ja’afar (ndugu yake Al Askari).
Anasema An-Nawbakhtiy (na huyu ni katika ‘ulamaa wakubwa wa Kishia) kuwa:
‘Baada ya kufa kwa Al-Hasan Al Askari, Mashia waligawika makundi kumi na nne’.
Na maudhui ya huyo ‘Imam Anayesubiriwa’, (anayedhaniwa kuwa ni mtoto wa Al Askari) yamo ndani ya kitabu chao kitukufu cha Al-Kaafiy yakikanusha kwake, yaani yanakanusha kuwepo kwa ‘Al Muntadhir’ Imamu anayesubiriwa, na ifuatayo ni mojawawapo ya riwaya nyingi zilizomo ndani ya kitabu hicho.
Riyawa inaeleza kuwa baada ya kifo cha Al-Hasan Al Askari, Sultani alitoa amri:
‘Kipekuliwe na kipigwe mihuri kila kitu ndani ya nyumba ya Al-Hasan’, na watu wakataka kujuwa juu ya habari za mwanawe, wakaletwa wanawake wanaofahamu vizuri juu ya mambo ya uzazi, wakaingia vyumbani mwa vijakazi vyake huku wakiwahoji na kuwauliza, na baadhi ya vijakazi hao wakasema kuwa wamesikia kuwa yupo mmoja kati ya vijakazi vyake ana mimba.
Wakamchukua kijakazi huyo na kumweka ndani ya chumba na kuwekewa mlinzi maalum pamoja na baadhi ya wanawake, kisha wakajitayarisha kwa ajili ya mazishi. Na masoko yalifungwa siku hiyo, na watu wa kabila la Bani Hashim pamoja na viongozi wote wakaondoka kuwenda mazikoni.’
Baada ya kufunikwa uso wake na kutolewa amri kuwa maiti ibebwe na kupelekwa nyumbani kwake na kuzikwa ndani humo katikati ya nyumba mahali alipozikwa baba yake, na baada ya kuzikwa, Sultani pamoja na waliokuwa wakisema kuwa (Al-Hasan Askari) alikuwa na mtoto, wakafanya kazi kubwa ya kutafuta na kuuliza majumbani, pakaamrishwa wangoje muda wa miaka miwili, na urithi usigawiwe mpaka walipohakikisha kuwa kijakazi yule hakuwa na mimba, na wala hapana kijakazi wake yeyote mwenye mimba, ndipo palipoamrishwa urithi ugawiwe kwa watu wawili, mama yake pamoja na Ja’afar ndugu yake Al-Hasan.
Haya yameandikwa ndani ya kitabu cha Al-Kaafiy, kitabu kinachoaminika na kukubaliwa na Mashia, yakithibitisha kuwa hajapata kuzaliwa mtoto wa aina hiyo na wala Al-Hasan Al Askariy hakuwa na mtoto, na hii ndiyo sababu urithi wake ukagawiwa baina ya mama yake na ndugu yake Ja’afar.’
Anasema An-Nawbakhtiy:
‘Al-Hasan alifariki dunia mwaka wa 260 akazikwa ndani ya nyumba yake na wala hajaacha mrithi wala hajaonekana kuwa na mtoto.’
(Haya ni maneno ya An-Nawbakhtiy ambaye pia anasema kuwa urithi wake Al-Hasan Al Askariy uligawiwa baina ya mama yake na ndugu yake Ja’afar), na akaendelea kusema: ‘na baada ya hapo wafuasi wake wakakhitalifiana na kugawika makundi kumi na nne. Na kundi la kumi na mbili na hawa ndio wanaojiita Al Imamiyah wakasema kuwa wao wanao ushahidi utokao kwa Allaah kuwa Al-Hasan Al Askariy alikuwa na mtoto, juu ya kuwa watu waliuliza na kutafuta lakini hapajaonekana mtoto yeyote.’
An-Nawbakhtiy katika kitabu cha ‘Firaq Ash-Shi’ah’ (Makundi ya Mashia) – ukurasa wa 108
Itikadi Za Kishia
Zituatazo Ni Itikadi Za Kishia Zinazokhitalifiana Kabisa Na Itikadi Za Masunni Na Kuhitalifiana Pia Na Waislamu Wengine. Itikadi hizi ni nyingi sana, lakini nitajaribu kuzitaja baadhi chache tu.
Itikadi Ya Kwanza
Itikadi ya ‘Ar-Raja-ah - nayo ni itikadi ya kufufuliwa na kurudi tena duniani baada ya kufa kabla ya siku ya Qiyaamah.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Kitabu Chake kitukufu ameikanusha itikadi hii ya kurudi tena duniani baada ya mtu kufa, aliposema:
لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾
Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha. (Ataambiwa) Laa hasha! Hakika hilo ni neno alisemaye yeye tu. Na nyuma yao kuna barzakh mpaka Siku watakayofufuliwa. [Al-Muuminuwn: 100]
Kwa hivyo kufufuliwa na kurudi tena duniani kabla ya siku ya Qiyaamah kumekanushwa na Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa ndani ya kitabu chake kitukufu, lakini mafundisho ya Kishia yanaitakidi kuwa Kufufuliwa huko kupo.
Imeandikwa na Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema: ‘Sunnah imetupa elimu ya vifo na elimu ya matatizo, na (pia imetupa sisi) neno la mwisho, na mimi ndiye Mwenye kurejea tena na tena na mwenye dola, na mimi ndiye mwenye fimbo na mwenye mnyama atakayezungumza na watu.’ Haya yamo ndani ya kitabu cha Al-Kaafiy Juzuu ya mwanzo ukurasa wa 198.
Alieyekifanyia tahakiki kitabu hiki Ali Akbar Al Ghafari anasema:
‘Neno ‘Mwenye kurejea tena na tena’, maana yake mwenye kufufuliwa tena na tena, yaani atarudi duniani mara nyingi baada ya kufa kwake.
Hapa Tutataja Majina Ya Imamu wa Madhehebu ya KiIthnaa ‘Ashariyah:
1. ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
2. Al-Hasan bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
3. Al-Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
4. ‘Aliy bin Al-Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
5. Muhammad bin ‘Aliy (maarufu kwa jina la ‘Al Baaqir’) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
6. Ja’afar bin Muhammad (maarufu kwa jina la ‘Asw-Swaadiq’) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
7. Musa bin Ja’afar (maarufu kwa jina ‘Al Kadhim’) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
8. ‘Aliy (maarufu kwa jina la ‘Ar-Ridha’ yaani ‘Aliy Ar-Ridhaa’) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
9. Muhammad (maarufu kwa jina la Muhammad Al Jawad) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
10. ‘Aliy (maarufu kwa jina la ‘Ali Al Hadi’) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
11. Al-Hasan bin ‘Aliy (maarufu kwa jina la Al Askari) (Radhwiya Allaahu ‘anhu)
12. Al Muntadhir (Mahd) ‘anayesubiriwa’ (na huyu ana majina mengi sana yakiwemo: Al Ghaib (asiyekuwepo), Al Muntadhir (anayesubiriwa), Al Khaif (mwenye kuogopa), na majina mengi mengine aliyebandikwa.
Na kabla ya kuendelea mbele kwa kuzitaja riwaya zilizopokelewa na Al-Kulayniy katika kitabu chake maarufu cha Al-Kaafiy, ningependa kukutanabahisheni jambo moja muhimu sana: nalo ni kuwa riwaya zote nitakazozitaja zilizoandikwa ndani ya vitabu vyao hivyo ni uongo waliosingiziwa imamu hawa wamesema. Kwani sisi tunawatakasa ‘Aliy bin Abi Twaalib na Al-Hasan na Al-Husayn na Ja’afar na Muhammad na Muwsaa na Aliy na Muhammad Al Jawad na wote hawa (Radhwiya Allaah ‘anhum) kuwa haiwezekani wao kuyatamka haya.
Sisi tunawatakasa wote hawa kuwa hawawezi kusema uongo kama huu waliowazulia, lakini ninachokusudia ni kuwa haya ndiyo yaliyomo ndani ya vitabu vyao.
Kwa hivyo anaeleza Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Ja’afar bin Muhammad anayejulikana kwa jina la Ja’afar Asw-Swaadiq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema:
‘Hakika Allaah aliwaambia Malaika: ‘Mubaki penye kaburi la Al-Husayn mpaka mtakapomuona akitoka (kutoka kaburini pake) hapo mumnusuru na mulie kwa ajili yake na kwa ajili ya yaliyokupiteni katika ushindi wake, kwani nyinyi mumehusishwa kwa ajili ya kumnusuru yeye na kumliliia.’
Kisha anaendelea kusema:
‘Malaika wakalia kwa huzuni kubwa kwa yale yaliyowapita kwa kukosa kumnusuru. Na atakapotoka (kaburini pake) watamnusuru (watapigana kwa ajili yake).’
Na ‘atakapotoka’, wanakusudia pale atakapotoka Al Mahdi Al Muntadhir wanayemsubiri maana itikadi yao ni kuwa wakati huo na Al-Husayn atafufuka na kurudi tena duniani, na hapo ndipo Malaika watakapomnusuru.
Wao wanaitakidi kuwa pale atakapokuja huyo wanayemsubiri, na imamu wote waliotangulia watatoka na kuwa pamoja naye.
Haya yamo ndani ya kitabu cha Al-Kulayniy kiitwacho Al-Kaafiy Juzuu ya kwanza ukurasa wa 284.
Na Itikadi yao hii ya mtu kufufuliwa tena hapa duniani ni itikadi tukufu sana kwao inayokwenda kinyume na maneno ya Allaah kama mlivyoona.
Itikadi Ya Pili
Kauli zao kuwa Swahaba wote walirtaddi (walitoka katika dini ya Kiislamu isipokuwa wachache sana).
Imesimuliwa na Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Muhammad bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na umaarufu wake ni Muhammad Al Baqer kuwa amesema: ‘Watu wote walirtaddi baada ya kufariki kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa watatu (tu).’ Ar-Rawdhah katika kitabu cha Al-Kaafiy ukurasa wa 246
Na imeandikwa humo pia kuwa Muhammad bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:
‘(Al Muhajirin) Watu wa Makkah na (Al Ansar) watu wa Madinah (wote) walitoka katika dini isipokuwa watatu (tu).’ Al-Kaafiy – Juzuu ya 2 ukurasa wa 244
Amesimulia huyo huyo Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Muhammad bin Ja’afar kuwa amesema:
‘Watatu Allaah hatosema nao siku ya Qiyaamah na wala hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo nao ni:
1- Kila anayeukataa uimamu wetu unaotoka kwa Allaah,
2- Na kila anayemkanusha Imamu aliyeletwa na Allaah
3- Na kila anayesema kuwa watu wawili hawa ni Waislamu.
Watu wawili wanaokusudiwa katika hadiyth hii ni Abu Bakr na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa). Na maana yake ni kuwa kila anayesema kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ni Waislamu basi Allaah hatosema naye wala hatomtakasa siku ya Qiyaamah na atapata adhabu iumizayo. Hadiyth hii imo katika kitabu cha Al-Kaafiy Juzuuu ya kwanza ukurasa 373
Itikadi Ya Tatu
Kauli yao kuwa kila asiyekuwa Shia ni kafiri – watu wote ni makafiri isipokuwa Mashia. Na yareti kama wangenyamaza hapo, bali wameendelea kusema kuwa: Kila asiyekuwa Shia ni kafiri na ni mtoto wa zinaa.
Amesema Bin Babawayh, na huyu ni katika ‘ulamaa wao wakubwa wa elimu ya hadiyth kuwa:
‘Kila anayemkanusha Imam anayesubiriwa, ukafiri wake ni mkubwa kupita hata wa Ibilisi – Yeyote anayemkanusha imamu ‘asiyeonekana’, ukafiri wake mkubwa kupita wa Ibilisi.’ Ikmalu ddin – Ukurasa 13
Ameeleza Al-Kulayniy katika Al-Kaafiykutoka kwa Muhammad al Baqer kuwa:
‘Watu wote ni watoto wa zinaa isipokuwa Mashia wetu.’ Na haya yamo katika Ar-Rawdhah - Al-Kaafiy ukurasa wa 239
Imesimuliwa na Al-Kulayniy katika Al-Kaafiy kutoka kwa Ar-Ridha kuwa amesema:
‘Hakuna Muislamu isipokuwa sisi na Mashia wetu.’ Juzuu ya 1 ukurasa wa 233
Anasimulia Al-Kulayniy katika Al-Kaafiy pia kutoka kwa Ja’afar bin Muhammad Asw-Swaadiq kuwa amesema:
‘Shetani huja na kukaa juu ya mwanamke sawa kama anavyokaliwa na mumewe, na hutenda kama anavyotendewa na mumewe na kumuingilia kama anavyoingiliwa.’
Muulizaji akauliza:
‘Vipi tutaweza kutofautisha?’
Yaani vipi mwanamke anaweza kujulikana iwapo ameingiliwa na shetani au ameingiliwa na mumewe?
Akajibu:
‘Kwa kutupenda na kutuchukia. Kila anayetupenda basi tone yake imetokana na binadamu, na kila anayetuchukia basi tone yake imetokana na shetani.’ Juzuu ya 5 katika kitabu cha Al-Kaafiy ukurasa wa 502
Amesema Ni’imatullah al-Jazaairiy – na huyu ni katika maulamaa wao wakubwa wa elimu ya hadithi katika wakati wake kuwa:
‘Sisi hatuko pamoja nao – (anakusudia Masunni) hatuko pamoja nao katika Allaah wala katika Nabiy wala katika Imamu, na hii ni kwa sababu wanasema kuwa Allaah wao ni yule ambaye Muhammad ni Nabiy wake na Abu Bakr ni Khalifa baada yake – na sisi tunasema: sisi hatumuabudu Allaah huyo wala Nabiy huyo, bali tunasema kuwa Allaah aliyemuumba Abu Bakr kuwa ni Khalifa wa Rasuli wake, huyo si Allaah wetu, na wala Nabiy huyo si Rasuli wetu.’ Amesema haya katika kitabu kiitwacho: ‘Al Anwar Al Nuamaniyah – Juzuu ya 2 ukurasa wa 278
Anasema Al-Huuru Al-’Aamiliy kuwa:
‘Ni’imatullah al-Jazaairiy ni mtu mwema, mwanachuoni, na mfanya tahakiki mkubwa sana.’
Amesema Al Khansariy:
‘Niamatullah alikuwa miongoni mwa wanachuoni wetu wakubwa sana na alikuwa bahari ya elimu katika wakati wake katika lugha ya kiarabu, na katika elimu ya Fiqhi na ya Hadiyth.’
Na Al Tijani ambaye ni mwanachuoni wao mkubwa katika zama hizi anasema:
‘Allaah aliyeridhika kumfanya Abu Bakr kuwa Khalifa baada ya Nabiy, sisi hatumtaki Allaah huyo.’
Ameyasema haya katika mhadhara alioufanya huko London na kaseti yake tumeihifadhi.
Itikadi Ya Nne:
Kauli yao kuwa Qur-aan imebadilishwa:
Itikadi ya Kishia ni kuwa Qur-aan imebadilishwa, au bora tuseme mafundiho ya madhehebu ya Kishia yanaitakidi kuwa Qur-aan imebadilishwa.
Anasema Ibni Hazm kuwa:
‘Mashia Imamiyah wote wa zamani na wa sasa wanaamini kuwa Qur-aan imebadilishwa na kuongezwa yasiyokuwemo na kupunguzwa ndani yake mengi pamoja na kubadilishwa mengi. ‘ Haya ni maneno ya Ibni Hazm
Anasema Ni’imatullah al-Jazairiy:
‘Habari ni nyingi sana bali ni nyingi kupita kiasi (mutawaatir) zinazotuthibitishia kuwa Qur-aan imebadilishwa maneno yake, mada zake, na irabu yake.’ Al-Anwaar an-Nu’umaniyyah – Juzuu ya 2 ukurasa 357
Kauli hizi zimesemwa na wingi miongoni mwa maulamaa wa Kishia akiwemo Al-Huuru Al-’Aamiliy anayejulikana kuwa ni miongoni mwa ‘ulamaa wakubwa.
Hebu tusikilize ‘ulamaa wa Kishia wanasema nini juu ya Al-Huuru Al-’Aamiliy.
Anasema Al Khunsariy:
‘Al-Huuru Al-’Aamiliy alikuwa katika ‘ulamaa wetu wakubwa sana waliotangulia na waliokuja baadaye na alikuwa bahari ya elimu’.
Ama Annuriy yeye anasema juu yake:
‘Al-Aamiliy alikuwa mfanya tahakiki, mwenye kuielewa vizuri elimu ya hadithi na mcha Allaah sana.’
Sasa hebu tumsikilize Al-Huuru Al-’Aamiliy mwenyewe anasema nini juu ya Qur-aan tukufu. Anasema Al-Huuru Al-’Aamiliy:
‘Juwa kuwa ukweli usio na shaka ndani yake kutokana na habari nyingi sana zilizotufikia ni kuwa hii Qur-aan tuliyonayo mikononi mwetu imebadilishwa kidogo baada ya kufa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wale walioikusanya baada yake wakapunguza mengi kati ya maneno yake na aya zake.’
Maneno kama haya yalitamkwa pia na Al Qumy na Al-Kulayniy na wengi miongoni mwa maulamaa wa Kishia akiwemo Ahmed bin Abi Twaalib Al Tubrusiy.
Anaendelea kusema Al-Aamiliy:
‘Na itikadi hii kuwa Qur-aan imepunguzwa ni katika mambo ya lazima kuamini kila mwenye kufuata madhehebu ya Kishia.’
Yote haya yamo ndani ya kitabu cha ‘Mira-atul Anwar’ ukurasa wa 36, Na maana yake ni kuwa Al-Aamiliy anaitakidi kuwa kila mwenye kufuata madhehebu ya kishia lazima aamini kuwa baada ya kufa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Qur-aan imepunguzwa na kuongezwa yale yasiyokuwemo.
Anasema Yusuf Al Baharani:
‘Kutokana na wingi wa riwaya hizi, inawezekana hata kuzitilia shaka sheria zote za dini kwani habari zote hizi zimepokelewa kupitia njia hiyo hiyo moja, mashekhe na wapokeaji wote ndiyo hao hao. Ikiwa watu hawa wameweza kufanya khiana kubwa, basi vipi watashindwa kuifanya khiyana hii ndogo?’
Unakusudiwa hapa uimamu wa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amana hiyo ni kubwa zaidi kupita dini yenyewe.
Durar al Najafiyah – ukurasa 294
Ama Adnan al Baharani yeye anasema:
‘Habari hizi (za kubadilishwa Qur-aan) ni nyingi sana hata haina haja ya kuziandika baada ya kuwa na uhakika kuwa pande zote mbili wamebadilisha kwa kuongeza na kupunguza (anakusudia na wao Mashia pia wamebadilisha), na kwa vile hata Swahaba na Tabiina wanayajuwa hayo vizuri, bali ijmai ya kundi lenye haki linayakubali hayo.’
Anakusudia kuwa Shia ndilo kundi lenye haki na kwamba ni wajibu kwao kuwa na itikadi hiyo. Shumus ad-Duriyah – 126
Anasema ‘Aliy bin Ahmad al-Kufiy:
‘Ulamaa wote wa riwaya na athar wamekubaliana kuwa Qur-aan hii iliyo mikononi mwa watu si kamili.’
Maneno haya haya yamesemwa na An-Nuur at-Twabrasiy katika kitabu chake maarufu sana kiitwacho ‘Faswlul Khitwaab’ – Ukurasa 27
Anasema An-Nuur at-Twabrasiy katika kitabu chake hicho maarufu kiitwacho ‘Faswlul Khitwaab fiy Tahriyfi Kitaab Rabbil Arbaab:
‘Miongoni mwa dalili kuwa Qur-aan imebadilishwa ni ule ufasaha wake mwingi katika baadhi ya aya na upuuzi ulio ndani ya baadhi ya aya.’
Katika kitabu chake hicho An-Nuur at-Twabrasiy ameziandika suwrah nyingi sana pamoja na aya anazodai kuwa zimeachwa au kubadilishwa, na hapa nitaandika baadhi chache ya sura na aya hizo:
Nitaanza na Suwrah maarufu waliyoipa jina la ‘Suratul wilayah’: anasema Attubrusiy kuwa sura hiyo ni kama ifuatavyo:
“ يأيها الذين آمنوا آمنوا بالنورين أنزلناهما يتلواني عليكم آياتي ويحذرانكم عذاب يوم عظيم نورا في بعضهما من بعض وأنا السميع العليم ، إن الذين يوفون بعهد الله ورسوله في آيات لهم جنات النعيم والذين كفروا من بعد ما آمنوا بنقضهم ميثاقهم وما عاهدهم الرسول عليه يقذفون في الجحيم ظلموا أنفسهم وعصوا وصية الرسول أولئك يسقون من حميم”
’Yaa ayuha lladhiyna amanu aaminu binnurayni anzalnahuma yatluwaani ‘alaykum ayaatiy wa yuhadhiraanikum ‘adhaabi yawmin ‘adhiym nuuran fiy ba’adhihima min baadhin wa anaa ssamiy’ul ‘aliym. Inna lladhiyna yuwafuwna bi’ahdi Llaahi wa rasuwlihi fiy ayatin lahum jannatun na’iym walladhiyna kafaruw mim ba’adi ma aamanuw binaqdhihim miythaqhim wama ‘aahad-hum arrasuwlu ‘alayhi yuqdhafuwna fil jahiym. Dhalamuw anfusahum wa ‘asaw wasiyat rrasuwl ulaaika yusqawna min hamiym.’
Haya yamo ndani ya vitabu vyao mashuhuri kama hicho nilichotangulia kukitaja cha Nuri Al Tubrusi, na pia mwanachuoni wao mwengine aitwae Abi Shahar Ashub na wengi miongoni mwa ‘ulamaa wa Kishia wameandika hayo.
Imepokelewa kuwa ‘Aliy bin ‘Abdillaah alipoisoma aya isemayo:
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ ..﴿١١٠﴾
maana yake ni: Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu;..[Aal-Imraan: 110]
Akasema Ja’afar Asw-Swaadiq: ‘Umma bora wanamuuwa Amiril muuminin na Al-Hasan na Al-Husayn alayhimaa-salaam?’
Na alipoulizwa: ‘Vipi niisome?’
Akajibu:
‘Isome hivi: ‘Kuntum khayra aimmatin’. Na maana yake: Nyinyi ni maimamu bora.’
Hata Suwrah Ash-Sharh wanasema imeteremshwa kama ifutavyo:
‘Alam nashrah laka swadrak – wawadhaana ‘anka wizrak – alladhiy anqadha dhwaharak - warafaana laka dhikrak - bi ‘Aliyyin suhrak.”
Hizi ni baadhi chache sana ya aya na sura wanazoitakidi kuwa zimebadilishwa. Na Nuri Attubrusi huyu katika kitabu chake ameandika faharasi ya Qur-aan yote kuanzia Suwrah Al-Baqarah mpaka Suwrah Ikhlaasw huku akizichambua aya anazosema kuwa zimebadilishwa.
Kilichobaki ni kumjuwa: nani huyu Nuri Attubrusiy aliyeandika kitabu akidai kuwa Qur-aan hii tuliyonayo imebadilishwa?
Anasema Abbas Al Qumiy mwandishi wa kitabu kiitwacho: ‘Alkuniya wal laqab:
‘An-Nuur at-Twabrasiyy ndiye Shekhe wa Waislamu – mwenye elimu ya Manabii na Rusuli – mwenye kuaminika – aalim aliyekamilika.’
Ama Agha Barzak Al Taharani katika kumsifia An-Nuur at-Twabrasiy anasema:
‘Imamu wa maimamu wa elimu ya hadithi na ni katika ‘ulamaa wakubwa wa kishia katika karne za mwisho na mkuu wa mashekhe wa kiislamu katika karne hii.’
Hivi ndivyo anavyosifiwa huyu aliyeandika kitabu akakiita: ‘Fasli l khitab fiy ithbat taharif kitab rabbi l arbab.
Na maana yake ni:
Kauli ya uamuzi juu ya kubadilishwa kwa kitabu cha Allaah.
Itikadi ya tano:
Kuvunja heshima ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
Mtu anaweza kushangaa! Vipi watavunja heshima ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wameleta hadiyth wanayodai kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:
‘Nilisafiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa hana mtumishi isipokuwa mimi, na alikuwa na upande mmoja tu wa shuka ya kujifunikia, na hakuwa na shuka nyengine isipokuwa hiyo na alikuwa amefuatana na Aishah, na Rasuli wa Allaah alikuwa akilala kati yetu mimi na Aishah na sote watatu tulikuwa tukijifunika kitambaa hicho hicho kimoja. Shuka moja tu (tukijifunikia sote watatu).
(Eti Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akilala kati na upande wake wa kulia akilala Aliy na upande wa kushoto akilala Aishah – Astaghfirullah!).
Anasema: ‘Anapoinuka Nabiy kwa ajili ya kusali, alikuwa akiivuta shuka kwa mkono wake na kuiacha iguse ardhi baina yangu na Aishah.’
Maana yake ni kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anapokwenda kusali alikuwa akiwaacha Aliy na Bibi Aishah wamelala huku wamejifunika upande mmoja wa shuka!!!
Haya yamo ndani ya kitabu chao maarufu kiitwacho ‘Bihaar al-Anwaar’, Juzuu ya 2 ukurasa 40.
Wakati huo huo katika kitabu cha Al-Kaafiy imeandikwa kuwa: ‘Atakapokutwa mwanamume na mwanamke wamejifunika upande mmoja wa shuka. Basi wahukumiwe hukmu ya waliozini’.
Wanasema haya, kisha wanaleta hadithi ya uongo kuwa Aliy na Aisha (Radhwiya Allaahu ‘anhu) walikuwa wakijifunika upande mmoja wa shuka, tena mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Itikadi Za Shia Ithnaa ‘ashariyah (ithnasheri) Juu Ya Maimamu Wao Kumi Na Mbili
Bila shaka Itikadi ya Kishia juu ya Imamu wao ni uvukaji wa mipaka yote ya Kiislamu.
Imepokelewa katika kitabu chao maarufu tena kinachoheshimiwa sana kiitwacho Al-Anwaar an-Nu’umaniyyah Juzuu ya 1 ukurasa 31 kuwa:
‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema:
‘Wa-Allaahi nilikuwa pamoja na Ibraahiym ndani ya ule moto na mimi ndiye niliyeufanya uwe baridi na salama, na nilikuwa pamoja na Nuwh ndani ya (lile) jahazi nikamuokoa asizame, na nilikuwa pamoja na Muwsaa nikamfundisha Taurati, na nilikuwa pamoja na ‘Iysaa nikamfanya aseme akiwa bado mtoto mchanga, nikamfundisha Injili, na nilikuwa pamoja Yusuf ndani ya shimo, nikamuokoa kutokana na hila za ndugu zake, na nilikuwa na Suleiman juu ya busati, nikautiisha upepo uweze kufuata amri yake.” Al-Anwaar an-Nu’umaniyyah Juzuu ya 1 ukurasa 31
Anasema Al-Kulayniy katika kitabu cha Al-Kaafiy kutoka kwa Ja’afar bin Muhammad kuwa amesema:
‘Kwetu sisi ipo elimu ya yaliyopita na yatakayokuja mpaka Qiyaamah kitakaposimama.’
Al-Kaafiy – Juzuu 1 ukurasa wa 239
Na anasema Al-Kulayniy:
Kutoka kwa wengi miongoni mwa sahibu zetu kutoka kwa Ahmed bin Muhammad kutoka kwa ‘Abdullaah bin Al Hajjal kutoka kwa Ahmed bin ‘Umar al Halaby kutoka kwa Abu Basiyr amesema:
‘Niliingia kwa Abu ‘Abdillaah nikamwambia: ‘Najitolea mhanga kwa ajili yako, nataka kukuuliza juu ya jambo. Yupo mtu anayesikia maneno yangu?” Abu ‘Abdillaah (na hapa anakusudiwa Ja’afar Asw-Swaadiq) akanyanyua pazia iliyokuwa baina yake na baina ya nyumba ya pili na kuangalia ndani yake, kisha akasema:
‘Ee babake Muhammad, uliza unachotaka?’
Anasema, akasema: ‘Najitolea mhanga kwa ajili yako! Mashia wetu wanazungumza kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) alimfundisha Aliy alayhi salaam mlango (wa elimu) unaofungua milango elfu (mingine)?’
Akasema Abu ‘Abdillaah:
‘Ee Aba Muhammad! Sisi pia tunayo Al Jaamiah na kipi kinachokujulisha ukaijuwa hii Al Jaamiah?’
Akaendela kusema: ‘(Huu) ni ukurasa, urefu wake dhiraa sabini kwa dhiraa ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimsomea kwa mdomo wake na huku (Aliy) akiandika kwa mkono wake wa kulia yote yaliyohalalishwa na yaliyoharamishwa na kila kinachohitajiwa na wanadamu hata uchokozi na kujichuna’.
‘Nikawambia: ‘Hii ndiyo elimu ya kweli’.
Akasema:
‘Hakika hii ni elimu na si ile. Kisha akanyamaza muda kidogo, kisha akasema:
‘Tunayo pia Al Jifr, na kipi kitakachokujulisha ukaijuwa hiyo Al Jifr? Hiki ni Chombo kilichotoka kwa Adam, ndani yake mna elimu ya Rusuli na ya waliousiwa, na elimu ya ‘ulamaa waliotangulia wa Bani Israil’.
Nikamwambia:
‘Hii ndiyo elimu ya kweli’
Akasema:
‘Hii ni elimu ya kweli na si ile’, kisha akanyamaza muda, kisha akasema:
‘Na kwetu pia tunao Msahafu wa Faatwimah Alayhaa-salaam, wanaujuwaje wao msahafu wa Faatwima?’
Nikamuuliza:
‘Ni kitu gani hiki kinachoitwa msahafu wa Faatwimah?’
Akasema:
‘Msahafu, ndani yake mna mfano wa Qur-aan yenu hii mara tatu! Wa-Allaahi hamna ndani yake yaliyomo ndani ya Qur-aan yenu hii hata herufi moja’.
Nikamwambia:
‘Na elimu ni ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)’
Akanambia:
Sisi kwetu tunayo elimu ya yaliyotangulia na yanayotokea na yatakayotokea mpaka siku ya Qiyaamah !!!!!
Al-Kaafiy – 239
Kuhusu ile kauli: ‘mfano wa Qur-aan yenu hii mara tatu’, katika riwaya nyengine wameandika kuwa: ‘Idadi ya aayah zilizomo ndani ya msahafu wa Faatwimah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ni elfu kumi na saba’, na sote tunaelewa kuwa idadi ya aayah za Qur-aan ni elfu sita na kidogo. Kwa hivyo ukizidisha mara tatu utapata karibu idadi hiyo.
Na ameeleza Al-Kulayniy katika Al-Kaafiy kutoka kwa Abu Naseer kuwa alimuuliza Ja’afar Asw-Swaadiq: “Kweli nyinyi mnaweza kufufua waliokufa na kuwawezesha vipofu kuona na kuponyesha wenye mabalanga?”
Akajibu:
‘Ndiyo.’
Al-Kaafiy – Juzuu 1 ukurasa wa 47
Kuhalalisha Damu Ya Masunni
Damu ya Masunni na mali zao ni halali katika itikadi za Kishia, lakini wanaisubiri fursa nzuri.
Katika vitabu vya historia vilivyoandikwa na maulamaa wao mbali mbali kama vile Naseer al Tusi na Ibni al Alqamiy na wengine yameandikwa yafuatayo:
‘Kutoka kwa Daud bin Farqad amesema: ‘Nilimuuliza Abu ‘Abdillaah alayhis- salaam: ‘Nini rai yako juu ya kuwauwa Al Nasib? (Masunni).’
Akasema:
‘Damu yao ni halali, lakini fanya Taqiyah, na utakapoweza kumuangushia ukuta au kumzamisha majini ili usiweze kupatikana ushahidi dhidi yako, basi fanya hivyo.’
Nikamuuliza: “Nini rai yako juu ya mali yake?”
Akasema: “Fanya utakavyo juu yake.”
Ilal al Sharaia – na Al-Anwaar an-Nu’umaniyyah – ukurasa wa 308
Anasema Al Tusiy, kutoka kwa Abu ‘Abdillaah kuwa alisema:
‘Chukuwa mali ya Al Nasib (Sunni) popote utakapoipata kisha utulipe na sisi khumsi yetu.’
(Khumsi ni zaka maalum wanadai kuwa wanapewa watu wa nyumba ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
Mayahudi Na Manasara Bora Kuliko Masunni?
Anasema Al Majlisiy katika Bihaar al-Anwaar kutoka kwa Abu ‘Abdillaah – Ja’afar bin Muhammad aliulizwa juu ya huyo Imam anayesubiriwa atakapotoka atawafanya nini Mayahudi na Manasara?, akajibu:
‘Atafanya amani nao kama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyofanya amani nao, na watatoa Jizya huku wakiwa dhalili.’
Nikamuuliza:
‘Na Masunni je? (Al Nasib)’
Akajibu:
‘Haiwezekani kwa aliyekwenda kinyume nasi katika dola yetu. Allaah keshatuhalalishia damu zao pale atakapotoka ‘Imamu wetu’ tunayemsubiri. Msidanganyike, siku atakapotoka msimamizi wetu Allaah atalipa kisasi chake na cha Nabiy wake na chetu sote.’
Bihaar al-Anwaar – Juzuu ya 48 ukurasa wa 376
Anasema huyo huyo Al Majlisi kuwa:
‘Hapana kilichobaki baina yetu na baina ya waarabu isipokuwa kuwachinja.’
Kisha akaashiria kwa mkono wake shingoni pake.
Bihaar al-Anwaar – Juzuu ya 52 ukurasa wa 349