Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kukaa Na Mtu Anayevuta Sigara Mpe Nasaha Asiposikia Ondoka

Kukaa Na Mtu Anayevuta Sigara Mpe Nasaha Asiposikia Ondoka

 

Imaam Ibn ‘Uthymiyn (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) anafafanua hilo.

 

“Ikiwa pembeni yako kuna mtu mvutaji wa sigara na akataka avute, basi mpe nasaha kwa upole, mwambie: “Ee ndugu yangu hili jambo ni haraam na wala si halaal kwako.”

 

Mimi ninadhania kuwa ukimnasihi kwa upole ataacha, kama walivyojaribu wenzetu na sisi pia tulijaribu hivyo, kama hakuacha kuvuta sigara, lililo wajibu kwako ni kuondoka hiyo sehemu.

 

 

Allaah (Subhaanhu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

 وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ

Na kwa yakini Amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayaat za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Au sivyo mtakuwa kama wao. [An-Nisaa: 140]

 

 

Lakini hii ni kama upo kwenye sehemu za mjumuiko. Ama kama utakuwa sehemu ya kazi na ukampa nasaha ikawa hataki kuacha, basi hakuna ubaya wewe kuendelea kubaki kwa sababu hii ni dharura na wala huwezi kuepukana nayo.

 

 

[Fataawaa Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn- Liqaau Bab Maftuwh (45)]

 

 

 

Share