Biskuti Za Chumvi

Biskuti Za Chumvi

 

 

VIPIMO                          

Unga - 3 Vikombe vya chai

Siagi   -  250 gms

Baking powder -   3 Vijiko vya chai

Mayai  -   2

Chumvi -  1 kijiko cha chai

Maziwa  -    1/2 Kikombe

Pilipili manga ya unga     1 Kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream).
  2. Tia Unga, baking powder, pilipili manga.
  3. Tia maziwa.
  4. Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda.
  5. Pika (bake) katika moto wa 350º C – usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.

 

 

Share