Skip to main content

Imaam Ibn Baaz: Kufukia Kucha Nini Hukmu Yake?

Kufukia Kucha Nini Hukmu Yake?

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

Alhidaaya.com

 Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema katika kujibu swali:

“Jambo hili (la kufukia kucha) halina asili (katika dini), mtu akikata kucha zake anaweza kuzitupa na hakuna neon, hivyo hakuna haja ya kuzifukia”

[Fataawaa Nuwr ‘Ala Ad-Darb (5/6)]