Imaam Ibn Baaz: Hedhi Nifaas: Anapopata Twahara Usiku Aswali Swalaah Zipi?

 

Hedhi Na Nifaas Anapopata Twahara Usiku Aswali Swalaah Zipi?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Amesema Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

 

“Pindi watakapoona (Twahara), ni juu yao upesi upesi kukosha kiasi kumuwezesha kuswali Maghrib na Ishaa wa usiku ule, kama ilivyotolewa fatwa kuhusu hilo na Jamaa miongoni mwa watu wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hali kadhalika wakitoharika wakati wa Alasiri basi yawapasa wao kufanya haraka kukoga ili waweze kuiswali Adhuhuri na Alasiri kabla ya kuzama jua”.

 

[Fataawaa Nuwr ‘ala Ad-Darb (516)]

 

 

 

 

Share