Skip to main content

Imaam Ibn Baaz: Mwanamke Kufanya Sajdah At-Tilaawah Bila Ya Kujifunika Kichwa Inajuzu?

Mwanamke Kufanya Sajdah At-Tilaawah Bila Ya Kujifunika Kichwa Inajuzu?

 Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

Alhidaaya.com

SWALI:

Je inajuzu kwa mwanamke kufanya Sajdatut-Tilaawah (Sijda Ya Kusoma Qur-aan) bila ya kujifunika kichwa?

JIBU:

“Akisujudu akiwa hajajifunika hakuna neno ni sawa, bali akijisitiri kama vile yupo kwenye Swalaah na akasujudu akiwa ni mwenye twahara ni bora zaidi.”

[Fataawa Nuwr ‘ala Ad-Darb (11352)]