Imaam Ibn Baaz: Ramadhwaan: Mwenye Swawm Ni Muhimu Asiache Sahuwr (Daku)

 

Mwenye Swawm Ni Muhimu Asiache Sahuwr  (Daku)

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Inampasa mwenye swawm asiache kabisa Sahuwr (daku) japo ale kidogo kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Amkeni kwa ajili ya (kula) Sahuwr kwani Sahuwr ni Baraka.”

 

Na baraka hii haipasi kupotea bali inampasa Muumini aitile himma japo kwa kitu kidogo cha chakula au tamar (tende) au maziwa ili imsaidie kwayo ‘amali  za mchana za Dini na za kidunia.”

 

 

www.binbaz.org.sa

 

 

Share