019-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji:Kula Kwa Mkono Wa Kulia, Na Kutomega Chakula Kilicho Mbele Ya Mwingine

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

Alhidaaya.com

 

Adabu Za Kula

 

019-Kula Kwa Mkono Wa Kulia

Na Kutomega Chakula Kilicho Mbele Ya Mwingine

 

 

 

 

2-3-  Kula Kwa Mkono Wa Kulia, Na Kutomega Chakula Kilicho Mbele Ya Mwingine Kama Wanakula Sahani Moja

 

 

Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

ذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ فَلْيَأْكُلْ بِيَمِيْنِهِ، وَإِذَا شَرِبَ فَلْيَشْرَبْ بِيَمِيْنِهِ، فَإِنَّ اَلشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِشِمَالِهِ، وَيَشْرَبُ بِشِمَالِهِ".

 

“Anapokula mmoja wenu, basi na ale kwa mkono wake wa kuume, na anapokunywa, basi na anywe kwa mkono wake wa kuume, na sababu ni kuwa shaytwaan anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2020), At-Tirmidhiy (1800) na Abu Daawuwd (3776)].

 

Na toka kwa ‘Amr bin Abiy Salamah, amesema:

 

"كُنْتُ غُلاَماً فِي حِجْرِ رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ ، وَكَانَتْ يَدِيْ تَطِيْشُ في الصَّحْفَةِ، فَقَالَ لِيْ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ‏ : يَا غُلاَمُ ! سَمِّ اَللَّهَ ، وَكُلْ بِيَمِيْنِكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيْكَ"، فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتِي بَعْدُ"‏.

 

“Nilikuwa kijana mdogo nikilelewa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mkono wangu ulikuwa ukitembea huku na kule kwenye sinia.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia:  “Ee kijana mdogo!  Sema “Bismil Laah” , kula na mkono wako wa kuume, na kula kile kilicho mbele yako”.  Na baada ya hapo, ukawa huo ndio ulaji wangu siku zote.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5376) na Muslim (2022)].

 

Share