08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Udhwhiyah: Mahala Pa Kuchinjia

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

الأُضْحِيَةُ

 

 Udhwhiyah  

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

08-Udhwhiyah: Mahala Pa Kuchinjia:

 

 

Mwenye kuchinja ameruhusiwa kuchinja sehemu yoyote ile baada ya Swalaatul ‘Iyd, ni sawa ikiwa nyumbani kwake au kwingineko.  Pia anaruhusiwa kuchinja katika sehemu ilikwoswaliwa ‘Iyd.  Jundub bin Suyfaan amesema:

 

"شَهِدْتُ الأَضْحَى مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ، فَلَمْ يَعْدُ أَنْ صَلَّى وَفَرَغَ مِنْ صَلاَتِهِ سَلَّمَ ، فَإِذَا هُوَ يَرَى لَحْمَ أَضَاحِيَّ قَدْ ذُبِحَتْ قَبْلَ أَنْ يَفْرُغَ مِنْ صَلاَتِهِ ، فَقَالَ : ‏ "‏ مَنْ كَانَ ذَبَحَ أُضْحِيَّتَهُ قَبْلَ أَنْ يُصَلِّيَ - أَوْ نُصَلِّيَ - فَلْيَذْبَحْ مَكَانَهَا أُخْرَى ، وَمَنْ كَانَ لَمْ يَذْبَحْ فَلْيَذْبَحْ بِاسْمِ اللَّهِ" 

 

“Nilihudhuria Al-Adhwhaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Hakufanya jingine lolote isipokuwa aliswali nasi, akaimaliza Swalaah na akatoa tasliym.  Kutahamaki akaona nyama za wanyama wa udhwhiyah waliochinjwa kabla hajamaliza Swalaah.  Akasema:  Aliyekuwa amedhwahi mnyama wake kabla hajaswali -au kabla hatujaswali- basi achinje badala yake mnyama mwingine.  Na ambaye bado hajachinja, basi achinje kwa kulitaja Jina la Allaah”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (1960) na An-Nasaaiy (7/214)].

 

Hadiyth hii inaonyesha kuwa walichinja katika eneo waliposwalia ‘Iyd.

 

Imestahabiwa kwa Imamu achinje mahala pa kuswalia ili watu wajue kwamba wakati wa kudhwahi ushaingia, lakini pia wajifunze kutoka kwake namna ya kuchinja.  Ibn ‘Umar amesema:

 

"كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَذْبَحُ وَيَنْحَرُ بِالمصَلَّى"

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anachinja katika sehemu ya kuswalia (‘Iyd)”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5552), Abu Daawuwd (2811), An-Nasaaiy (7/213) na Ibn Maajah (3161)].

 

 

Share