Skip to main content

09B-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: لِبَاسُ المَرْأَةِ Kivazi Cha Mwanamke13-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Kivazi Cha Mwanamke: Inajuzu Mwanamke Kupakiwa Nyuma Ya Mwanaume Ambaye Ni Maharimu Wake

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

لِبَاسُ المَرْأَةِ

Kivazi Cha Mwanamke 

Alhidaaya.com 

013-Inajuzu Mwanamke Kupakiwa Nyuma Ya Mwanaume Ambaye Ni Maharimu Wake:

Ni kwa Hadiyth ya Anas ambaye amesema: 

"كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَقْفَلَهُ مِنْ عُسْفَانَ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى رَاحِلَتِهِ، وَقَدْ أَرْدَفَ صَفِيَّةَ بِنْتَ حُيَىٍّ، فَعَثَرَتْ نَاقَتُهُ فَصُرِعَا جَمِيعًا"

“Tulikuwa tunarudi pamoja na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) toka ‘Usfaan.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amempanda ngamia wake na amempakia nyuma yake (mkewe) Swafiyyah bint Huyay.  Na mara ghafla ngamia wake akajikwaa na wote wawili wakaanguka chini.  [Al-Bukhaariy (3085) na Muslim (1345)].