18-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Kivazi Cha Mwanamke: Kuonyesha Mapambo Kwa Watoto Ambao Hawafahamu Chochote Kuhusu Mambo Ya Wanawake Wala Uchi Wao

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

لِبَاسُ المَرْأَةِ

Kivazi Cha Mwanamke 

 

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

018-Kuonyesha Mapambo Kwa Watoto Ambao Hawafahamu Chochote Kuhusu Mambo Ya Wanawake Wala Uchi Wao:

 

Allaah Amesema:

 

"أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ"

 

“Au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake”.  [An-Nuwr: 31].

 

Ibn Kathiyr amesema:  “Yaani, kutokana na umri wao mdogo, hawafahamu hali za wanawake na nyuchi zao, au maneno yao ya siri za ndani.  Ikiwa mtoto ni mdogo hafahamu chochote katika hayo, basi hakuna ubaya kuingia kwa wanawake.  Lakini kama ni barobaro au anakaribia ubarobaro kiasi ambacho anaweza kuyajua hayo na kuyatambua, au anaweza kutofautisha kati ya mwanamke mbaya na mrembo, basi asiruhusiwe kuingia kwa wanawake”. 

 

Yanayoashiria hayo ni Hadiyth ya Jaabir:

 

"أَنَّ أُمَّ سَلَمَةَ اسْتَأْذَنَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْحِجَامَةِ ، فَأَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا طَيْبَةَ أَنْ يَحْجُمَهَا، قَالَ: حَسِبْتُ أَنَّهُ  قَالَ: كَانَ أَخَاهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ أَو غُلَامًا لم يَحْتَلِمْ."

 

“Kwamba Ummu Salamah alimwomba ruhusa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) afanye hijama.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru Abu Twaybah amuumike.  Anasema:  Nadhani kama alisema:  Alikuwa ni kaka yake wa kunyonya au kijana mdogo ambaye hajabaleghe”.  [Muslim (2206), Abu Daawuwd (4105) na Ibn Maajah (3480)].

 

 

 

Share