06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Wanawake Ambao Ni Haramu Kuwaoa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

06-Wanawake Ambao Ni Haramu Kuwaoa:

 

Wanawake hawa Allaah Ta’aalaa Amewataja katika Aayaah hizi tatu:

 

"وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلا حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا  وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا"

 

“Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita.  Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu•  Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati zenu (mama wakubwa na wadogo), na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia●  Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa).  Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita.  Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.  Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.  Ni Shariy’ah ya Allaah kwenu.  Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini.  Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib.  Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya kukamilika ya wajibu.  Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.”  [An-Nisaa: 22-24]

 

Wanawake hawa walioharamishwa wako aina mbili:

 

1-  Walioharamishwa kuwaoa milele.  Hawa mwanaume haruhusiwi kuwaoa abadani.

 

2-  Walioharamishwa kwa muda.  Hawa mwanaume haruhusiwi kuwaoa wanapokuwa katika hali maalum, na hali hii inapoondoka, hapo wanahalalika.

 

 

 

Share