03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe 2- Atulie Nyumbani Kwake, Asitoke Ila Kwa Ruksa Ya Mumewe
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
02: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe 2- Atulie Nyumbani Kwake, Asitoke Ila Kwa Ruksa Ya Mumewe:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ"
“Na bakieni majumbani mwenu, na wala msionyeshe mapambo na uzuri kwa ajinabi kujishaua kama zama za ujahili”. [Al-Ahzaab: 33]
Sheikh wa Uislamu amesema: “Si halali kwa mke kutoka nyumbani kwake bila idhini ya mumewe. Na kama atatoka bila idhini, basi anakuwa amegomea haki ya mume, amemwasi Allaah na Rasuli Wake, na anastahili adhabu”. [Majmuw’ul Fataawaa (32/281)]
