04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 3- Amkubalie Tendo La Jimai Kama Atataka

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com

 

 

 

03:  Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe:  3- Amkubalie Tendo La Jimai Kama Atataka:

 

Tendo la jimai ni haki mke ampatie mumewe ikiwa hali yake inaruhusu.  Kama hairuhusu kwa kuwa mgonjwa, au kachoka sana, au hajisikii vizuri, basi anaweza kukataa, na ni lazima mume naye achunge hali ya mkewe.  Kama hana lolote, basi anakuwa ni mwenye kumwasi Mola wake na anastahiki laana kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأَتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ فَأَبَتْ فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا لَعَنَتْهَا الْمَلَائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ"

 

“Mume akimtaka mkewe kitandani (kwa jimai) na mke akakataa, halafu mume akalala na hasira dhidi yake, basi Malaika watamlaani hadi kupambazuke”.  [Al-Bukhaariy (3237) na Muslim (1436)]

 

 

Share