05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 4-Asimruhusu Yeyote Kuingia Nyumbani Kwa Mumewe Ila Kwa Idhini Yake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com

 

 

 

04-Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe:  4-Asimruhusu Yeyote Kuingia Nyumbani Kwa Mumewe Ila Kwa Idhini Yake:

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anawaambia akina mama:

 

"وَإِنَّ لَكُمْ عَلَيْهِنَّ أَلاَّ يُوطِئْنَ فُرُشَكُمْ مَنْ تَكْرَهُونَ "

 

“Na kwamba haki yao wao kukufanyieni nyinyi ni kwamba wasimuingize nyumbani kwenu yeyote msiyetaka aingie humo”.  [Swahiyh Muslim (1218)]

 

Na anasema tena Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"وَلاَ تَأْذَنِ المَرْأَةُ فِي بَيْتِ زَوْجِهَا وَهُوَ شَاهِدٌ إِلاَّ بِإِذْنِهِ"

 

“Na mwanamke asiruhusu (kuwepo mtu) katika nyumba ya mumewe naye yupo isipokuwa kwa idhini yake”.  [Swahiyh Muslim (1026)]

 

Hili linachukulika kwa yule ambaye mke hajui kama mumewe anaridhika uwepo wake nyumbani.  Lakini kama atajua kwamba mume anaridhika, basi hakuna ubaya kumruhusu kama atakuwa ni katika watu wanaofaa kuingia kwake, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.  

 

 

Share