06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 5-Asifunge Swawm Ya Sunnah Ilhali Mumewe Yuko Ila Kwa Ruhusa Yake:
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
05: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 5-Asifunge Swawm Ya Sunnah Ilhali Mumewe Yuko Ila Kwa Ruhusa Yake:
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا يَحِلُّ لِلْمَرْأَةِ أَنْ تَصُومَ وَزَوْجُهَا شَاهِدٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ"
“Si halali mwanamke kufunga ilhali mumewe yuko ila kwa idhini yake”. [Al-Bukhaariy (5195), At-Tirmidhiy (782) na Ibn Maajah (1761)]
