07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 6-Asitumie Mali Yake Isipokuwa Kwa Idhini Yake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
06: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 6-Asitumie Mali Yake Isipokuwa Kwa Idhini Yake:
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا تُنْفِقُ امْرَأَةٌ شَيْئًا مِنْ بَيْتِ زَوْجِهَا إِلَّا بِإِذْنِ زَوْجِهَا"
“Mwanamke asitoe chochote cha nyumba ya mumewe ila kwa ruhusa yake”. [Abu Daawuwd (3565), At-Tirmidhiy (670), Ibn Maajah (2295). Sanad yake ni Hasan]
