09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 8-Amlinde Kwa Kujichunga Yeye Mwenyewe, Watoto Wa Mumewe Na Mali Yake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
08: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 8-Amlinde Kwa Kujichunga Yeye Mwenyewe, Watoto Wa Mumewe Na Mali Yake:
Allaah Ta’alaa Amesema:
"فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ"
Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. [An-Nisaa: 34]
At-Twabariy akiifasiri aayah hii amesema: “Yaani, wanajihifadhi wenyewe wakati waume zao wanapokuwa hawapo, kwa kuzilinda tupu zao na mali za waume zao”.
Nyuma tumeitaja Hadiyth hii isemayo kuhusu mwanamke bora zaidi isemayo:
"الَّتي تُطيْعُ زَوْجَهَا إِذَا أَمَرَ، وَتَسُرُّهُ إِذَا نَظَرَ، وَتَحْفَظُهُ فِي نَفْسِهَا وَمَالِهِ"
“Ni yule anayemsikiliza mumewe anapomwamrisha, anamfurahisha anapomtazama, na anamlinda kwa kujichunga yeye mwenyewe na mali ya mumewe”. [Hadiyth Swahiyh. An-Nasaaiy (6/68)]
