Skip to main content

10H(i)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (i) Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: Asimsimbulie Kama Atatumia Mali Yake Kwa Ajili Yake Na Watoto Wake

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

Alhidaaya.com

11:  Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 11-Asimsimbulie Kama Atatumia Mali Yake Kwa Ajili Yake Na Watoto Wake:

Kusimbulia kunaharibu thawabu na ajri kutoka kwa Allaah Anayesema:

"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ"

“Enyi walioamini!  Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia”.  [Al-Baqarah: 264]