13-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 12-Aridhike Kwa Kidogo Na Atosheke Nacho, Na Wala Asimbebeshe Yaliyo Juu Ya Uwezo Wake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
12: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 12-Aridhike Kwa Kidogo Na Atosheke Nacho, Na Wala Asimbebeshe Yaliyo Juu Ya Uwezo Wake:
Allaah Ta’alaa Amesema:
"لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا"
“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah. Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa. Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi”. [At-Twalaaq: 7]
