14-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 13-Asifanye Lolote Linalomuudhi Au Kumkasirisha
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
13: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 13-Asifanye Lolote Linalomuudhi Au Kumkasirisha:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تُؤْذِي امْرَأَةٌ زَوْجَهَا فِي الدُّنْيَا إِلَّا قَالَتْ زَوْجَتُهُ مِنَ الْحُورِ الْعِينِ: لَا تُؤْذِيهِ قَاتَلَكِ اللَّهُ، فَإِنَّمَا هُوَ عِنْدَكِ دَخِيلٌ يُوشِكُ أَنْ يُفَارِقَكِ إِلَيْنَا"
“Hakuna mwanamke yeyote anayemkera mumewe hapa duniani, isipokuwa mke wake mmoja katika mahurul-‘ayn humwambia: Usimsumbue, Allaah Akulaani, huyo kwako ni mgeni wa kupita tu, karibuni atakuacha aje kwetu”. [At-Tirmidhiy (1184) na Ibn Maajah (2014) kwa Sanad Hasan]
