16-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 15-Awe Na Hima Ya Kuendelea Kuishi Naye Hadi Mwisho, Na Asiombe Talaka Isipokuwa Kwa Sababu Za Kisharia
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
15: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 15-Awe Na Hima Ya Kuendelea Kuishi Naye Hadi Mwisho, Na Asiombe Talaka Isipokuwa Kwa Sababu Za Kisharia:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَيُّمَا امْرَأَةٍ سَأَلَتْ زَوْجَهَا طَلَاقًا فِي غَيْرِ مَا بَأْسٍ فَحَرَامٌ عَلَيْهَا رَائِحَةُ الْجَنَّةِ"
“Mwanamke yeyote anayemdai mumewe talaka bila kuwepo madhara yoyote, basi ni marufuku kwake harufu ya Pepo”. [Hadiyth Swahiyh. At-Tirmidhiy (1199), Abu Daawuwd (2209) na Ibn Maajah (2055)]
