17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe:16-Mumewe Akifa Amkalie Eda Kwa Muda Wa Miezi Minne Na Siku Kumi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com

 

 

16:  Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 16-Mumewe Akifa Amkalie Eda Kwa Muda Wa Miezi Minne Na Siku Kumi:

 

Mwanamke aliyefiwa na mumewe wa ndoa sahihi, ni lazima akae eda kwa muda wa miezi minne na siku kumi, ni sawa ikiwa alimuingilia au hakumuingilia, au ni katika wanaopata hedhi au waliokatikiwa.  Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا"

 

“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wajisubirishe wenyewe (kwa kukaa eda) miezi minne na siku kumi”.  [Al-Baqarah: 234]

 

 

Share