17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Asieneze Siri Zake Au Kutaja Kasoro Zake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
16: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 13-Asieneze Siri Zake Au Kutaja Kasoro Zake:
Kutaja siri za mke kwa watu wa nje ni haramu na hususan ikiwa siri zenyewe zinahusiana na maisha yao ya unyumba. Na dhambi inakuwa kubwa zaidi ikiwa siri yenyewe inahusiana na tendo la jimai.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ مِنْ أَشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللَّهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ الرَّجُلَ يُفْضِي إِلَى امْرَأَتِهِ وَتُفْضِي إِلَيْهِ ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا ".
“Hakika miongoni mwa watu wenye hadhi mbaya zaidi mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah, ni mtu anayemvaa mkewe kimwili na mkewe akamvaa, kisha akaja kuelezea siri yake kwa watu”. [Muslim (1437) na Abu Daawuwd (4870)]
