02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mke Zaidi Ya Mmoja: Masharti Ya Kuoa Mke Zaidi Ya Mmoja
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
تَعَدُّدِ الزَّوْجّاتِ
Mke Zaidi Ya Mmoja
02: Masharti Ya Kuoa Mke Zaidi Ya Mmoja:
1- Awe mtu na uwezo wa kufanya uadilifu kati yao.
Ni kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً"
“Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu”. [An-Nisaa: 03].
2- Ajijengee kinga ya kumlinda asije kufitinika akapoteza Haki za Allaah kwa sababu yao.
Ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ"
“Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao”. [At-Taghaabun: 14]
3- Awe na uwezo wa kuwatosheleza kimwili na kimahitaji.
Na hii ni ili wasivutike kwenda kwenye yaliyoharamishwa na machafu, kwani Allaah Hapendi mambo kama hayo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ، مَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمُ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ"
“Enyi rika la vijana! Atakayeweza miongoni mwenu kupata gharama za kuolea na kuendeshea maisha, basi na aoe”. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ"
“Na wajizuie (yaliyoharamishwa) wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah Awatajirishe kwa Fadhila Zake”. [An-Nuwr: 33]
