04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Kunyoa Kichwa Cha Mtoto Na Kutoa Swadaqah Ya Silver Ya Uzito Wa Nywele Zake Na Kumtahiri

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa:

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

04:   Kunyoa Kichwa Cha Mtoto Na Kutoa Swadaqah Ya Silver Ya Uzito Wa Nywele Zake Na Kumtahiri:

 

Toka kwa Anas bin Maalik:

 

"أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِرَأْسِ الحَسَنِ والحُسَيْنِ يَوْمَ سَابِعِهِمَا، فَحُلِقَا، وَتَصَدَّقَ بِوَزْنَهِ فِضّة"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru Al-Hasan na Al-Husayn waletwe kwake siku ya saba ya kuzaliwa kwao, akawanyoa, na akatoa swadaqah silver ya uzito wa nywele zao”.  [Hadiyth Swahiyh.  At-Tirmidhiy (1519), Al-Haakim (4/237) na Al-Bayhaqiy (9/304)]

 

Angalizo:

 

Haijuzu kunyoa kichwa cha mtoto sehemu na kuacha nyingine mfano wa panki, denge na kadhalika.  Toka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:

 

"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْقَزَعِ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kunyoa denge (panki)”.  [Al-Bukhaariy (5920) na Muslim (113)]

                                                           

 

Kumfanyia Sunnah (Kumtahiri):

 

Kuna baadhi ya Hadiyth zilizotajwa kuhusiana na kusuniwa kumfanyia mtoto wa kiume sunnah siku ya saba ya kuzaliwa kwake.  Lakini sanadi za Hadiyth hizi ni dhwa’iyf, ingawa zinaweza kuzatitiana zenyewe kwa zenyewe.  Kati yake ni:

 

"أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَقَّ عَنِ الحَسَنِ وَالحُسَيْنِ وَخَتَنَهُمَا لِسَبْعَةِ أَيَّام"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwafanyia Al-Hasan na Al-Husayn ‘aqiyqah na akawatahiri siku ya saba (ya kuzaliwa)”.  [At-Twabaraaniy katika As-Swaghiyr (891) na Al-Bayhaqiy (8/324).  Sanad yake ni dhwa’iyf] 

 

 

 

Share