Zingatio: Ewe Mtenda Madhambi

 

Zingatio: Ee Mtenda Madhambi

 

Naaswir Haamid

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Ee mwenye kufanya dhambi usiaminishe kwamba hutolipwa kwa madhambi yako na kwamba hutoyaona matokeo ya ubaya wa dhambi hiyo. Na kule kuifatilia kwako hiyo dhambi, basi dhambi yake ni kubwa kuliko huko kukifanya hicho kitendo cha dhambi.

 

 

Na kutokuona haya pale unapofanya kitendo cha dhambi wakati Malaika yuko kuliani kwako na mwengine kushotoni kwako ni kubaya zaidi kuliko hiyo dhambi.

 

 

Na kuifanya kwako hiyo dhambi huku ukiwa unacheka wala hujali nini Allaah Keshakutayarishia kwa ajili ya dhambi yako hiyo, ni kubaya kuliko hiyo dhambi.

 

 

Na kule kucheka kwako wakati ukifanya kitendo cha dhambi ni kubaya zaidi kuliko kuitenda hiyo dhambi.

 

 

Na kule kuhuzunika kwako pale unapokosa kukifanya kitendo cha dhambi ni kukubwa zaidi kuliko hiyo dhambi yenyewe.

 

 

Ee mtenda madhambi upepo unaogopa pale unapotikisa mlango wakati unapokuwa katika hali ya kukifanya kitendo cha dhambi wakati moyo wako wala haushtuki wala kujali kuwa Rabb wako Anakuona, ni kubaya zaidi kuliko hiyo dhambi.

Share