Sitta Shawwaal: Anaweza Kufunga Swawm Za Sunnah Katika Mwezi Wa Shawwaal?

Anaweza Kufunga Swawm Za Sunnah Katika Mwezi Wa Shawwaal?

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

assalam alaikum warahmatu llahi wabarakatuhu,je inafaa kufunga sunna ya jumatatu na alhamisi katika mwezi huu wa shawwali?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Unaweza kufunga Sunnah za Jumatatu na Alkhamiys na hata Swiyaam za Ayyaamul-biydhw (tarehe 13, 14, 15 mwezi wa Hijri). Na unaweza kufunga siku hizo pamoja na Sitta Shawwaal kwa sharti iwe umeshamaliza kulipa deni lako la Ramadhwaan hivyo utakuwa unapata thawabu za Sitta Shawwaal  na za siku hizo In Sha Allaah.

 

Kwa faida ziyada bonyeza kiungo kifuatacho:

 

Sita Za Shawwaal Na Swawm Nyinginezo Baada Ya Ramadhaan  

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share