Sitta Shawwaal: Kulipa Deni Kwanza Au Kufunga Sita Shawwaal
Kulipa Deni Kwanza Au Kufunga Sita Shawwaal
SWALI:
Je infaa kwa mwanamke kulipa siku zake katika siku sita za mwanzo wa shawal halafu ndio nifunge hizo sita baada ya kulipa deni? Nilifamishwa na jamma kwa haifai kufunga kamwe katika siku sita kwa mwanamke aliekuwa na deni, eti ni kungoja mpaka sita zieshe ndio nione kulipa na kufunga sita za shawal. Tafadhali naomba ufafanuzi.
Shukran
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Swali lako mwanzo limefahamika na jibu ni kwamba hivyo ndivyo khaswa inavyotakiwa kwamba mtu alipe kwanza deni lake la Ramadhaan kisha ndio afunge Sita Shawwaal.
Ama kusema haifai kufunga kamwe katika siku sita, kama unakusudia kusema haifa kufunga katika mwezi huu wa Shawwaal, ndio mtu alipe deni, basi hivyo sio sahihi. Bali ni hivi ifuatavyo:
1) Ikiwa mtu ana deni na anataka kufunga Sita Shawwaal basi kwanza lazima afunge deni lake mwanzo katika mwezi huu wa Shawwaal ili awahi kupata siku Sita za mwezi huu wa Shawwaal kabla ya kumalizika.
2) Ikiwa mtu hana nia ya kufunga Sita Shawwaal na analo deni la swawm na anataka kulilipa deni, basi ni khiari yake kama atapenda kulilipa deni katika mwezi huu wa Shawwaal au mwezi wowote mwingine. Lakini akilipa (akifunga) katika mwezi wa Shawwaal deni lake haimaanishi kwamba atapata fadhila za kufunga Sita Shawwaal kwani hivyo ni kulipa deni tu.
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na faida ziyada kuhusu hukmu za Sitta Shawwaal:
- Fataawa Mbali Mbali Kuhusu Kulipa Deni Na Kufunga Sita Shawwaal
- Hukmu Ya Kufunga Ijumaa Ikiwa Ni Siku Ya 'Arafah Au 'Ashuraa
- Hukumu Ya Kufunga Siku Ya Jumamosi Pekee Na Inapoangukiwa Siku Ya 'Arafah Au 'Ashuraa
- Ufafanuzi Wa Thawabu Za Sita Kama Kufunga Mwaka Mzima
- Kulipa Deni La Ramadhaan Na Sita Shawwaal
- Inafaa Kufunga Swawm Za Naafil (Sunnah) Kabla Ya Kulipa Deni La Ramadhaan?
- Kufunga Ijumaa Na Jumamosi Katika Sita Ya Shawwaal Yafaa
- Ufafanuzi Wa Thawabu Za Sitta Kama Kufunga Mwaka Mzima
Na Allaah Anajua zaidi.